Advertisements

Tuesday, November 22, 2016

CONGRATULATIONS HOPE NA KEMIE KWA KUPATA UBARIKIO


Hope na Kemie ni watoto wa Mao Luangisa na Sophie watoto wao wapendwa walipata ubarikio siku ya jumapili ndani ya kanisa la United Lutheran huko Mt Vernon. NY Ubarikio ni mafundisho ambayo yanatolewa kwa vijana ambao sasa wameshapata upeo wa kuweza kupokea mafundisho ya kiroho,kimwili na hata maisha kwa ujumla.Kwa kawaida vijana hao ni wale ambao wameshafikisha miaka 12 na kuendelea.Nia hasa ni kutaka kuwafundisha vijana kama neno la mithali 22:6 “mlee mtoto katika njia impasayo naye hatoiacha hata akiwa mzee”

Ubakio ni mafundisho ambayo yamekuwa ni misingi wa imani ,kwa mfano unafundishwa kuwa mda wowote unaweza kusali,ukiwa unatembea,upo kitandani unataka kulala,nk mafundisho kama”kwa nini Mungu katika nafsi tatu”,”Sakramenti takatifu ya meza ya Bwana”,”Neema ya Msalaba” na mengine mengi

Kwa hivyo nia hasa ni kumpa kijana mafundisho akiwa bado mdogo kama waswaili wanavyosema samaki mkunje angali mmbichi ili mafundisho hayo yatakayomsaidie mtoto katika imani yake na safari yake ya kwenda mbinguni 

Sophie na mume wake Mao Luangisa wakiwa ndani ya kanisa, kwa taswira zaidi nenda soma zaidi

No comments: