Advertisements

Tuesday, November 29, 2016

HALMASHAURI ZINAZOZALISHA MKAA ZATAKIWA KUANZISHA MASHAMBA YA MITI- MAJALIWA

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais – Muungano na Mazingira Mh. January Makamba akiongea wakati wa warsha ya Wadau juu ya kujadili mikakati ya kupunguza matumizi ya mkaa Nchini iliyofanyika jijini Dar es Salaam. Warsha hiyo imeandaliwa na Ofisi ya Makamu wa rais.
Waziri wa Maliasili na Utalii Prof. Jumanne Maghembe ambaye alimuwakilisha Mgeni Rasmi Mh. Waziri Mkuu Mh. Kassim Majaliwa akisoma hotuba ya ufunguzi ya warsha ya kujadili mikakati ya kupunguza matumizi ya Mkaa kwa niaba ya Waziri Mkuu jijini Dar es Salaam le. Warsha hiyo imeandaliwa na Ofisi ya Makamu wa rais.
Sehemu ya Wadau mbalimbali waliohudhuria warsha ya kujadili mikakakti ya kupunguza matumizi ya mkaa iliyoandaliwa an Ofisi ya Makamu wa Rais wakimsikiliza Mwakilishi wa Mgeni Rasmi Mh. Profesa Jumanne Mghembe (hayupo pichani).
Mmojawapo ya watoa mada Bwana Mhandisi Estomih Sawe kutoka TaTeDO akiwasilisha mada juu ya njia za kuwezesha upungazaji wa matumizi ya mkaa kwa jamii aktika warsha iliyoandaliwa na Ofisi ya Makamu wa Rais na kuhudhuriwa na Wadau mbalimbali jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Wafadhili na Wjumbe wa warsha hiyo wakifuatilia kwa umakini uwasilishwaji wa mada katika warsha hiyo.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amezitaka Halmashauri zote zinazozalisha mkaa Nchini kuanzisha mashamba ya miti kwa ajili ya kupata nishati hiyo, ili mkaa usitokane tena na miti ya asili. Hayoyalisomwa katika hotuba yake iliyosomwa kwa niaba yake na Waziri wa Maliasili na Utalii Prof. Jummanne Maghembe wakati wa ufunguzi wa warsha ya kujadili mikakati ya kupunguza matumizi ya mkaa iliyoandaliwa na Ofisi ya Makamu wa Rais jijini Dar es Salaam.

Aliongeza kuwa kila Halmashauri iandae mwongozo wa uzalishaji, matumizi na biashara ya mkaa katika mashamba yatakayoanzishwa na kwamba program za kupanda miti zifanyike wakati wa msimu wa mvua ili kuhakikisha miti yote inapona na uwepo mpango wa kuzuia mifugo kuharibu miti itakayopandwa. Pia alisisitiza kila mfanayabiashara wa mkaa ahakikishe lazima ana shamba la miti kwa ajili ya nishati ya mkaa na vibali vya biashara hiyo vitolewe kwa masharti haya.

Akiongea wakati wa kumkaribisha Mgeni Rasmi , Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais-Muungano na Mazingira, Mh. January Makamba alisema kuwa Ofisi ya Makamu wa Rais itashirikiana bega kwa bega na Wadau ili kupunguza utumiaji wa matumizi ya mkaa. Alitanabaisha kuwa Ofisi yake imeandaa shindano la kutafuta mkaa mbadala na mshindi wa kwanza atapata milioni 300.

Ofisi ya Makamu wa Rais kwa kushirikiana na Wadau wa maendeleo wameandaa warsha kwa Wadau ili kuwapa elimu na kuwaongezea uelewa juu ya athari za matumizi ya mkaa na kuchanganua mbinu za kutafuta mbadala wa matumizi ya mkaa.

1 comment:

Anonymous said...

Nilitegemea serikali ingepiga marufuku matumizi ya mkaa na kupromote matumizi ya coal charcoal na gas. Resources ambazo tunazo na zina doda tuu