Advertisements

Thursday, November 17, 2016

HAPI ATAJA MAENEO YA MAGULIO KINONDONI


Na Bashir Nkoromo
Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, imeainisha maeneo ya magulio kwa ajili ya wafanyabiashara ndogo ndogo, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa agizo la Rais John Magufuli kuzitaka mamlaka zinazohusika kutenga maeneo ya wafanyabiashara hao kabla ya kuwatimua katika maeneo yasiyoruhisiwa.


Akizungumza na waandishi wa habari leo Ofisini kwake, Mkuu wa Wilaya hiyo, Salum Hapi, ameyataja maeneo hayo kuwa yapo katika kata za Kinondoni, Bunju, Msasani, Mabwepande, Kunduchi na Kata ya Wazo.


Hapi amesema, vitu vitakavyoruhiswa kuuzwa kwenye magulio hayo ni bihaa za sokoni, vyombo vya nyumbani, nguo mpya na mitumba, viatu, urembo, na kwamba kwa ujumla ni bidhaa ambazo hutumiwa na watu katika maisha ya kila siku.


Ametaja mpangilo unaotakiwa kwenye magulio hayo kuwa ni, kupangwa eneo moja bidha zinazofanana, viwepo vyoo vya muda, na uafi wa eneo la gulio ambao utasimamiwa na Mtendaji Mwenyewe wa eneo husika.

MPANGILIO NA RATIBA KAMILI YA MAGULIO HAYONo comments: