Advertisements

Friday, November 25, 2016

Jike Dume Atingisha, Ashikwa Kwa Kuwatapeli Wanaume Wenzake

Image result for Ivan Bebeto
Kijana Ivan Bebeto (28), Duniani kuna mambo.
Stori: Hamida Hassan na Mtandao, WIKIENDA
Uganda: DUNIANI kuna mambo! Kijana Ivan Bebeto (28) yamemkuta ya kumkuta baada ya hivi karibuni kushikiliwa kwenye Kituo cha Polisi cha Katwe jijini Kampala kwa madai ya kuwatapeli wanaume kwa kujifanya ni mwanamke ‘jike dume’ huku akivaa mavazi ya kike, kujipodoa na  kuvaa mawigi.
Habari zilizotua kwenye dawati la Wikienda zinadai kuwa, jike dume huyo hufanya biashara katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki hususan jijini Kampala (Uganda), Bujumbura (Burundi), Nairobi (Kenya) akitokea pia Dar es Salaam (Tanzania).
ANATUMIA JINA LA QUEEN 

Kwa mujibu wa chanzo, Ivan baada ya kujibadili na kuwa katika mwonekano wa mwanamke hujiita Queen kwa maana ya jina la kike, wanaume wengi wanaomjua akiwa hivyo humwita kwa jina hilo.
“Uzuri wake si rahisi kutambua kuwa ni mwanamke  kwani  amekuwa akijipamba, anatumia manukato ya kike na anapoingia kwenye klabu za usiku, hujichanganya na warembo wengine waliotoka kwenda viwanja ili kutofahamika kuwa ni mwanaume,” kilisema chanzo.
SASA MKASA WAKE WA KUKAMATWA NI HUU
Mkasa mzima wa kukamatwa kwa jike dume huyo hivi karibuni nchini Uganda ulianza pale alipokutana na  mwanaume mmoja ambaye hakujulikana jina mara mmoja.
Mwanaume huyo alitokewa na ‘Queen’, akaingia mzimamzima na baada ya mazungumzo, aliamua kumlipa kabisa chake na kumtaka waende kwenye nyumba ya wageni ‘gesti’ moja jijini Kampala kwa ajili ya kumalizana kama makubaliano yao yalivyo.
AKATAA KWENDA NYUMBA YA WAGENI
Inadaiwa kuwa, baada ya malipo hayo ambayo kiasi cha pesa hakijatajwa, Bebeto alikataa kwenda nyumba ya wageni na kumtaka mteja wake huyo waende kwenye nyumba aliyodai kuwa, huwa anahifadhia mizigo yake huku akimsisitizia kuwa atafurahi kwa sababu watakuwa wote usiku mzima.
ASHTUKIWA
Ikazidi kudaiwa kuwa, kutokana na mtazamo wake, mwanaume huyo alimshtukia Bebeto kwamba anaweza kuwa mtu mbaya, ndipo aliamua kuwajulisha polisi wa kituo hicho ambao walifika haraka sana kumkamata.
MAMBO HADHARANI
Baada ya tukio la kukamatwa, ndipo aligundulika kuwa, Bebeto ni kidume na si mwanamke na hajawahi kuwa mwanamke tangu azaliwe hali ambayo iliwashangaza na  polisi wenyewe.
WATU KIBAO KITUONI
Habari za mwanaume kukamatwa kwa madai ya kujibadili kuwa mwanamke ili apige pesa zilisambaa kwa kasi, watu wa eneo hilo wakakusanyika kituoni Katwe kwa ajili ya kumshuhudia Bebeto na kila aliyemuona hakuamini kutokana na uzuri aliokuwa nao lakini alipovua wigi alionekana kichwa chake halisi ingawa hata kama asingekuwa na wigi bado ilikuwa vigumu kumjua ni ‘meni’ mpaka kumchunguza.
AFUNGULIWA RB
Polisi wa Kituo cha Katwe waliamua kumfungulia kesi kijana huyo yenye faili la kumbukumbu REF65/04/11/2016 ambapo ameshikiliwa mpaka gazeti hili linakwenda mtamboni.
GPL

No comments: