Tanga, KIWANDA Cha Saruji Cha Simba Cement kimeijengea shule ya Msingi ya Kange vyumba viwili vya madara na madawati 50 pamoja na matundu mawili vya vyoo vyote vikiwa na thamani zaidi ya shilingi milioni 76.
Msaada huo umekuja kupunguza kero ya wanafunzi kurundikana darasa moja na wengine kukaa chini jambo ambalo hupunguza ufahamu wa wanafunzi darasani.
Akizungumza katika hafla fupi ya makabidhiano, Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Thobias Mwailapwa, alisema msaada huo uwe mfano kwa makampuni mengine na wadau wa elimu lengo likiwa ni kuondokana na changamoto ya baadhi ya shule inazokabiliana nazo.
Kwa upande wake, Mkuu wa Rasilimali watu kiwanda cha Saruji cha Simba Cment, Anna Malambugi, alisema kiwanda hicho moja ya sera zake ni kusaidia jamii ikiwemo, Elimu, Afya na Mazingira.
Nae Mwalimu mkuu wa Shule hiyo, Debora Danniel, alisema awali walikuwa wakiwaweka wanafunzi 120 darasa moja kufuatia uhaba wa madarasa.
Alisema kwa msaada huo utaondosha kero ya wanafunzi kurundikana darasa moja na kuwaomba wadau wa elimu kuisaidia shule hiyo katika Nyanja mbalimbali ikiwemo miundombinu yamaji na uchakavu wa majengo.
Mwisho
Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Thobias Mwailapwa akifungua moja milango ya vyumba viwili ya madarasa shule ya msingi Kange Tanga, anaemtazama ni Afisa Fedha Pitter De Jagger na kulia ni Mkurugenzi wa jiji la Tanga, Daudi Mayeji.
Afisa Uhusiano kiwanda cha Saruji cha Simba Cement cha Tanga, Noor Mtanga, akiwakabidhi madawati 50 wanafunzi wa shule ya msingi ya Kange pamoja na majengo mawili na vyoo vyenye matundu mawili vyote vikiwa na thamani zaidi ya shilingi milioni 76, nyuma kulia ni Mwenyekiti wa mtaa wa Kasera, Aidan Munis na kulia ni mwalimu mkuu wa shule hiyo, Debora Mzava.
Mkuu Rasiliwamali watu kiwanda cha Saruji cha Simba Cement cha Tanga, Anna Mwalambuji akiwakabidhi madawati 50 wanafunzi wa shule ya msingi ya Kange kufuatia uhaba wa madawati shule hiyo pompja na kuwakabidhi jengo la vyumba viwili na vyoo vyenye matundu mawili vyote vikiwa na thamani zaidi ya shilingi milioni 76.
0655 902929
No comments:
Post a Comment