Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akiangalia mfereji wa Tandale ambao umearibiwa kutokana wananchi ambao wamekuwa wakitupataka katika mfereji huo, leo jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akiteta na Mlemaavu ambaye amemkuta katika eneo la uwanja wa fisi akinywa pombe za kienyeji na kumsihi aache kunywa pombe hizo, leo jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akiwa ameongozana na Kamanda wa kanda maalum, Simon Siro kugonga nyumba za wadada ambao uufanya biashara ya kujiuza katika eneo la uwanja wa fisi, leo jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akiwa na Kamanda wa kanda maalum, Simon Siro wakiangalia bia ambazo zinauzwa uwanja wa fisi zikiwa zimekwisha muda wake kwa ajili ya matumizi ya Binadamu, leo jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, akiteta na mmoja wa wakazi wa jiji la eneo la Tandale.
Wakazi wa Tandale wakiwa wamesimama kumsubiri mkuu wa mkoa.
Mmoja wa mkazi wa jiji ambaye amekutwa na kamera yetu akiwa anagonga kwenda kwenye chumba cha wanawake wanaojiuza. Picha zote na Emmanuel Massaka, Globu ya jamii.
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akisalimiana na dereva wa daladala katika kituo cha Tandale kwa mtogole, leo jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam ,Paul Makonda akiangalia barabara ya Tandale inayounganisha na Mwananyamala ambayo imekuwa apitiki kwa uraisi kwa kipindi chote kutokana mashimo ya yaliyopo,leo jijini Dar es Salaam.
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii
MKUU wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ameaidi kutafuta wafadhili watakaoweza kununua nyumba za uwanja wa fisi hili kuweza kufuta biashara ya ngono katika eneo hilo.
Makonda amesema hayo maema leo alipokuwa akiendelea na ziara yake ya Dar es Salaam mpya katika Wilaya ya Kinondoni eneo la Tandale na kujionea mwenyewe kwa macho namna gani biashara ya ngono inavyofanywa na watu kunywa pombe za kienyeji .
“atuwezi kuacha kuona vijana wetu wakipote na kupotoka kimaadili kwa watu kujenga majengo na madanguro ambayo yana amasisha biashara ya ngono katikati ya makazi hivyo nitatafuta wawekezaji kua kununua eneo hilo hili kuondoa biashara hiyo” Amesema Makonda.
1 comment:
Wape fedha ya kuendesha maisha yao. Hali ni tete wapeni biashara za kufanya.
Hivyo ndivyo Viwanda tulivyolenga.??
Post a Comment