Advertisements

Tuesday, November 29, 2016

PRO. OLE GABRIEL AMEWAASA WADAU WA MICHEZO KUSHRIKIANA ILI KUONGEZA FURSA ZA AJIRA KWA VIJANA.

 Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel akiongea na baadhi ya viongozi wa vyama vya michezo leo mkoani Mbeya  (hawapo pichani) ikiwa ni moja ya malengo ya ziara yake ya kikazi mkoani humo. Kulia ni Kaimu Afisa Michezo mkoa ambaye pia ni Afisa Michezo Jiji la Mbeya, Joyce Mwakifwamba
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel akikiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa vyama vya michezo leo mkoani Mbeya . (Picha na Eleuteri Mangi-WHUSM, Mbeya)


Na Eleuteri Mangi-WHUSM, Mbeya
Wadau wa michezo mkoni Mbeya wametakiwa kuendeleza mshikamano walionao ili kuifanya sekta ya michezo kuwa chanzo cha kuongeza fursa za ajira kwa vijana pamoja na wataalamu wengine wa michezo.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel amesema hayo leo jijini Mbeya alipokuwa akiongea na baadhi ya viongozi wa vyama vya michezo mkoani humo ikiwa ni moja ya malengo ya ziara yake ya kikazi mkoani humo.
“Nimefurahishwa na mkoa wa Mbeya kuwa na mipango ambayo imewafanya vyama vya michezo kuendeshwa bila kuwa na migogoro, hii ni hatua nzuri imenipa moyo, mkishikamana vizuri mtafanikiwa sana katika malengo yenu ya michezo” alisema Prof. Ole Gabriel.
Ili kuhakikisha michezo inakuwa na tija kwa mkoa wa Mbeya na taifa, Prof Ole Gbriel ametaka viongozi hao kuwa na mkakati wa kimkoa wa kubadilisha fikra za watu katika michezo na kutambua kuwa zipo fursa nyingi katika michezo yote bila kubagua aina ya mchezo.
Awali akitolea ufafanuzi baadhi ya masuala ya michzo, Prof. Ole Gabriel ameataka wadau hao kutambua kuwa michezo inaanzia katika ngazi ya chini, hivyo ni wajibu wao kuendeleza michezo kwa kubadili fikra za wazazi, vijana, walezi kuipenda michezo kwa kuwa inamchango mkubwa katika ajira, pato la familia pamoja na uchumi wa taifa.
Akimkaribisha Katibu Mkuu Prof. Ole Gabriel, Kaimu Afisa Michezo mkoa ambaye pia ni Afisa Michezo Jiji la Mbeya, Joyce Mwakifwamba amesema kuwa Serikali ya mkoa inaendelea kushirikiana na wadau wa michezo yote kwa kuzingatia michezo ni ajira, udugu katika kujenga umoja wa michezo kimkoa na taifa.
Akizunguzia mpira wa miguu, Katibu Msaidizi Chama cha Mpira wa Miguu Mbeya (MREFA) Lucas Kubaja amesema kuwa mpira wa miguu unachezwa kuanzia ngazi ya chini, wilaya zote hadi mkoa.
Kubaja ameongeza kuwa mkoa unapokuwa na timu nyingi za michezo mbalimbali katika ligi za michezo hiyo inasaidia kuongeza fursa za kiuchumi kwa wakazi wa mkoa wa mbeya kunapokuwa na timu zinazokuja kucheza mechi zao kwenye ligi husika.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti wadau hao wa michezo wamemweleza Katibu Mkuu mwenye dhamana ya michezo kuwa michezo mingi mkoani Mbeya inakabiliwa na changamoto ya kutokuwa na viwanja vya michezo hatua ambayo inarudisha nyuma ukuaji wa michezo mbalimbali.
Vyama nya michezo vilivyoshiriki mkutano huo huo ni mpira wa miguu (MREFA), mpira wa pete (CHANETA), mpira wa kikapu, chama cha makocha, riadha, vishale pamoja na  pool table.
Aidha,katika ziara hiyo,  Katibu Mkuu pia ametembelea  Ofisi za kanda ya Nyanda za Juu Kusini za Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) pamoja na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kwa lengo la kujionea namna wanavyofanya kazi ya kuimarisha mawasiliano katika kanda hiyo. 

No comments: