Waziri wa Mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Augustine Mahiga akizungumza na Waandishi wa habari juu ya ujio wa Rais wa Zambia kwa ziara ya siku tatu.
Afisa uhusiano wa Wizara wa Mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mindi Kasiga, akizungumza na waandishi wahabari
Baadhi ya wafanyakazi wa wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki wakifatilia mkutano huo.
Waziri wa Mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki,Balozi Augustine Mahiga akizungumza na Waandishi wa habari juu ya ujio wa Rais wa Zambia kwa ziara ya siku tatu kulia ni Balozi wa Tanzania nchini Zambia, Grace Mujuma.
Balozi wa Tanzania nchini Zambia, Grace Mujuma akizungumza na Waandishi wa Habari juu ya mikataba ya Zambia na Tanzania juu ya wafanyakazi wa TAZARA.
Mkurugenzi wa idara ya Afrika wa Wizara ya Mambo ya nje na ushirikiano wa frika Mashariki, Balozi Samweli Shelukindo akizungumza na waandishi wa Habari
Na Humphrey Shao,Globu ya Jamii
RAIS wa Zambia Edgar Lungu anataraji kuwasili nchini kwa ziara ya siku tatu nchini Tanzania kwa mwaliko wa Rais John Pombe Magufuli kuanzia tarehe 27 mpaka 29.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Waziri wa Mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Augustine Mahiga, amesema ziara hiyo ambayo inataraji kukuza na kuimarisha uhusiano uliopo kati ya nchi hizi mbili.
“katika ziara hii Rais wa Zambia atatembelea Bandari ya Dar es Salaam, Reli ya Tazara na mradi wa bomba la mafuta la TAZAMA amabalo limetoka hapa nchini mpaka Zambia” amesema Balozi Mahiga.
Amemaliza kwa kusema kuwa ni vyema watu wakaanza kuina kariakoo kama sehemu ambayo inasaidia kukuza mahusiano yetu kati ya Tanzania na Zambia kwa kuwezesha wanawake zaidi 1000 ambao hufika sokoni hapo kila siku.
No comments:
Post a Comment