Mkurugenzi Msaidizi wa Fedha na Mipango, Servus Sagday akielezea madhumuni ya warsha ya siku tatu ya Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDG's) kwa Maofisa Maendeleo ya Jamii na Maofisa Mipango nchini iliyofadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kufungua warsha hiyo inayoendelea mjini Dodoma katika ukumbi wa mikutano Hazina ndogo.
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Serikali za Mitaa kutoka Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Miriam Mmbaga amewataka maofisa Maendeleo ya Jamii na Maofisa Mipango nchini kufanya kazi kwa uzalendo ili Tanzania iweze kufikia malengo ya maendeleo endelevu (SDG’s) ifikapo mwaka 2030 kama ilivyokusudiwa.
Kauli hiyo aliitoa mjini Dodoma wakati wa ufunguzi wa warsha ya malengo endelevu kwa maafisa hao kutoka kanda ya Ziwa ambayo imeandaliwa na Wizara ya Fedha na Mipango .
Alisema uhamasishaji kuhusu malengo haya ni matokeo ya Nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa kukamilisha utekelezaji wa Malengo ya Milenia yaliyokamilika mwaka 2015.
Alisema Mpango wa maendeleo endelevu utatekelezwa kati ya mwaka 2015 hadi 2030, hivyo pia na unajulikana kama agenda 2030 na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kama mwanachama wa Umoja wa Mataifa pia iliridhia utekelezaji wa malengo hayo.
Alisema katika utekelezaji wa mpango huo lazima maafisa hao wawe na uzalendo kwa kufanya kazi kwa maadili.
“Bila kubadili fikra zao malengo hayo hayataweza kufikiwa, tufanye kazi kwa bidii ili ifikapo mwaka 2030 tuweze kujipima na kuweza
kushangilia kwa kufikia malengo ya maendeleo endelevu 17 ambayo yamejikita kwenye sekta mbalimbali,”alisema Mmbaga.
Alisema changamoto iliyopo kwasasa ni namna ya kufikia malengo hayo, hivyo ni lazima kuwa tayari kubadilika katika kufanya kazi na kutafsiri mambo.
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Serikali za Mitaa kutoka Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Miriam Mmbaga akifungua warsha ya siku tatu ya Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDG's) kwa Maofisa Maendeleo ya Jamii na Maofisa Mipango nchini inayoendelea katika ukumbi wa mikutano Hazina ndogo mjini Dodoma chini ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP).
“Tutakuwa tunavutana, tunaangushana na itatupotezea muda wa kufikia kwenye malengo haya lakini kikubwa ni lazima tukubali malengo ni ya kwetu na yapo kwa ajili yetu sisi wenyewe ili mwisho wa siku tuweze kuyafikia,”alisema.
Aliwahimiza kuwa na moyo wa uzalendo ili kufikia malengo hayo katika utatuzi wa changamoto mbalimbali zilizopo ikiwemo miundombinu.
“Lazima tutambue watumishi wa umma ni jeshi ambalo linatakiwa kupigana na maadui wale ambao wanatuathiri kijamii na kiuchumi na tuna maadui watatu ujinga, maradhi na umaskini, wakati wanapopigana na maadui waliopo kwenye malengo hayo na sisi tuunganishe na hawa maadui watatu,”alisema.
Alisema inawezekana ikapangwa mipango mbalimbali lakini kama hawatabadili fikra zao na hawapo tayari kufanya kazi ili kufikia malengo hayo kazi itakuwa ni ngumu.
Alibainisha tayari miongozo ya bajeti imeshatumwa kwenye mikoa hivyo kwa mujibu wa miongozo hiyo waangalie namna ya kupanga shughuli, miradi ambayo itajikita kufikia maelngo endelevu 17 ya Kitaifa na kidunia.
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) -Idara ya Uchumi, Dr. Wilhelm Ngasamiaku akitoa mada kuhusu Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDG's) na mchakato wake katika warsha ya siku tatu ya Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDG's) kwa Maofisa Maendeleo ya Jamii na Maofisa Mipango nchini inayoendelea katika ukumbi wa mikutano Hazina ndogo mjini Dodoma chini ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP).
Mkufunzi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Idara ya Uchumi, Dr. Joel Silas akitoa mada kuhusu uhusiano wa Maendeleo Endelevu (SDG's) na mpango wa maendeleo wa miaka mitano kwenye warsha ya siku tatu ya Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDG's) kwa Maofisa Maendeleo ya Jamii na Maofisa Mipango nchini inayoendelea mjini Dodoma katika ukumbi wa mikutano Hazina ndogo chini ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP).
Afisa kutoka Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Eva Ruhago akifafanua jambo kwa washiriki wa warsha ya siku tatu ya Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDG's) inayoendelea katika ukumbi wa Hazina ndogo mjini Dodoma chini ya ufadhili wa UNDP.
Pichani juu na chini sehemu ya washiriki wakitoa maoni wakati wa majadiliano katika warsha ya siku tatu ya Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDG's) kwa Maofisa Maendeleo ya Jamii na Maofisa Mipango nchini inayoendelea mjini Dodoma katika ukumbi wa mikutano Hazina ndogo chini ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP).
Pichani juu na chini ni sehemu ya Maofisa Maendeleo ya Jamii na Maofisa Mipango kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa ikiwemo Mikoa ya Kagera, Kigoma, Mara, Geita, Simiyu, Shinyanga na Mwanza wanaoishiriki warsha hiyo ya siku tatu yenye lengo la kufikisha ujumbe kwa watu wengi zaidi ili kutimiza kaulimbiu ya Malengo hayo isemayo "Hakuna atakayeachwa nyuma" inayolenga kujenga msingi wa malengo shirikishi yanayodhamiria kuleta maendeleo chanya kwa wote.
Mgeni rasmi Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Serikali za Mitaa kutoka Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Miriam Mmbaga (walioketi katikati) katika picha ya pamoja na Maofisa Maendeleo ya Jamii na Maofisa Mipango kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa ikiwemo Mikoa ya Kagera, Kigoma, Mara, Geita, Simiyu, Shinyanga na Mwanza wanaoshiriki warsha hiyo ya siku tatu inayoendelea mjini Dodoma chini ufadhili wa UNDP
No comments:
Post a Comment