Advertisements

Monday, November 21, 2016

WAZIRI WA UTAMADUNI NA SANAA WA AFRIKA YA KUSINI ATEMBELEA MAZIMBU CAMPUS MKOANI MOROGORO NA KUTEMBELEA MAKABURI YA WAPIGANIA UHURU WA AFRIKA YA KUSINI

Waziri wa Utamaduni na Sanaa wa Afrika ya Kusini Mhe. Nathi Mthethwa (aliyenyoosha mkono) akiangalia moja ya makaburi ya waliopigania uhuru wa nchi yake yaliyopo Mazimbu Campus Mkoani Morogoro.
Mkurugenzi wa SUA Solomon Mazimbu Campus Prof.Yasinta Muzanila(kulia) akitoa maelezo kwa Waziri wa Utamaduni na Sanaa wa Afrika ya Kusini Mhe. Nathi Mthethwa(kushoto) kuhusu Mazimbu campus na kumbukumbu zilizopo wakati Waziri huyo alipotembelea eneo hilo liliopo Mkoani Morogoro ambalo wapigania uhuru wa Afrika ya Kusini walilitumia katika harakati za kupigania uhuru wao na ukombozi wa bara la Afrika kwa ujumla.
Waziri wa Utamaduni na Sanaa wa Afrika ya Kusini Mhe. Nathi Mthethwa akisalimiana na Mkurugenzi wa SUA Solomon Mazimbu Campus Prof.Yasinta Muzanila alipowasili kutembelea eneo lililopo Mkoani Morogoro ambalo wapigania uhuru wa Afrika ya Kusini walilitumia katika harakati za kupigania uhuru wao na ukombozi wa bara la Afrika kwa ujumla
Waziri wa Utamaduni na Sanaa wa Afrika ya Kusini Mhe. Nathi Mthethwa akiwa katika eneo lililowekwa sanamu ya Rais wa kwanza Afrika ya Kusini Hayati Nelson Mandela kama ukumbusho wa wapigania uhuru wa Afrika ya Kusini Mazimbu Mkoani Morogoro.

No comments: