Advertisements

Monday, November 21, 2016

ZIARA YA MAKONDA WILAYA YA KIGAMBONI

Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza na wananchi katika eneo la barabara ya vumbi, hatua chache kutoka Daraja la Mwalimu Nyerere wilayani Kigamboni, baada ya wananchi kusimamisha msafara wake, wakitaka kujua hatma ya kipande hicho cha Kilometa 1.5, ambacho kiliachwa bila kuwekwa lani wakati wa ujenzi wa Daraja hilo.
Makonda ambaye alikuwa mwishoni mwa ziara yake ya siku mbili katika wilaya hiyo, leo, Jumapili, Novemba 20, aliwaahidi wananchi kuwa kipande hicho ambacho kimeonyesha kuwa kero, kitawekwa lami katika ujenzi utakaoanza wiki mbili zijazo kuanzia leo.
"Hili jambo limelisikia, na mimi kwa kuwa ni mwakilishi wa Rais Wetu Dk. John Magufuli, kwa mamlaka yake, nawaahidi kuwa kipande hiki serikali itakiweka lami na ujenzi utaanza wiki mbili zijazo. Haiwezekani Daraja zuri kama hili zilizinduliwe halafu kipande hiki kibaki kuwa hivi", alisema Makonda.
Alisema, fedha za ujenzi wa kipande hicho kwa kiwango cha lami, zipo na mkandarasi huyo, hivyo kilichobaki ni maandalizi madogomadogo tu ambayo siyo kikwazo.
Mapema wananchi kwa nyakati tofauti walilalamika kwamba, kuachwa kwa kipande hicho kumesababisha adha hasa ya vumbi na pia magari kadhaa kuharibika kutokana na makorogo yaliyopo katika kipande cha barabara hiyo.
Kabla ya kuzungumza na wananchi katika eneo hilo, Makonda alianza ziara yake kwa kukagua miti iliyopandwa darajani wakati wa kampeni ya mti wangu, iliyofanyika Oktoba mwaka huu jijini Dar es Salaam. ENDELEA NA PICHA ZAIDI ZA ZIARA HIYO
Baadhi ya viongozi waliokuwa katika msafara wa Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, wakitazama moja ya ramani zinazohusu uboreshaji wa miundombinu a mzingira katika wilaya ya Kigamboni. Kulia ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida na Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Temeke Sikunjema Yahya.

DAS wa wilaya ya Kigamboni Rahel Mhando akimsikiliza mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida aliyekuwa akimuuliza jambo, wakati msafara wa Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, uliposimamishwa na wananchi hatua chache kutoka daraja la mwalimu Nyerere, ili kujua hama ya kipande cha kilometa 1.5 kilichosalia bila kuwekwa lami. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Temeke Siknjema Yahya

DAS wa wilaya ya Kinondoni, Edward Mpogolo akijadili jambo na mmoja wa Wakurugenzi wa wilaya ya Kigamboni wakati msafara wa Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, uliposimamishwa na wananchi hatua chache kutoka daraja la mwalimu Nyerere, ili kujua hama ya kipande cha kilometa 1.5 kilichosalia bila kuwekwa lami
 
Baadhi ya wananchi wakifuatilia Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda alipokuwa akizungumza na wananchi waliosimamisha msafara wake hatua chache kutoka daraja la mwalimu Nyerere, ili kujua hama ya kipande cha kilometa 1.5 kilichosalia bila kuwekwa lami

Baadhi ya wananchi wakishangilia Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda alipokuwa akizungumza na wananchi waliosimamisha msafara wake hatua chache kutoka daraja la mwalimu Nyerere, ili kujua hama ya kipande cha kilometa 1.5 kilichosalia bila kuwekwa lami

KIBADA
Mkuu wa mkoa wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizugumza na wananchi katika eneo la Kibada, wilayani Kigamboni wakati wa ziara hiyo. Makonda alisikiliza kero mbalimbali ikiwemo ucheleweshwaji wa malipo kwa waliolengwa kuhama kupisha eneo serikali ilikopima viwanja kwa ajili ya makazi. Pia Makonda alizungumzia suala la bodaboda akihimiza Polisi kuendelea kuwakamata wale wanaoukiuka sheria ikiwemo kutovaa helmeti
Wananchi wa Kibada wakimsikiliza Makonda
"USIULIZE EMBE KIBADA", Mkazi wa Kibada akimsikiliza Makonda huku akiendelea na biashara yake ya embe. Kibada ni moja ya maeneo maarufu kwa embe za kila aina Dar es Salaam.

VISA VYA BODABODA KIBADA WAKATI MAKONDA HAJAONDOKA ENEO HILO 
Mwenyendesha bodaboda huyo ambaye hakuwa amevaa helmet huku pikipiki yake imesheheni mzigo, aliwapita trafiki kwa salama na amani bila kukamatwa.

DAMPO
Askari Polisi akimvalisha vizuri buti mkuu wake, wakati msafara wa Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ulipokuwa ukikagua eneo linalokusudiwa kujengwa dampo la kisasa, katika eneo la Ligato, wilayani Kigamboni. Hii inadhihirisha kwamba kufika katika eneo hilo, ilikuwa patashika kutokana na umbali na barabara isiyopitika vizuri 
Eneo lilaokusudiwa kujengwa dampo alilo kagua Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda katika eneo la Ligato, wilayani Kigamboni
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akipata maelezo kuhusu eneo linalokusudiwa kujengwa dampo la Kisasa katika eneo la Ligato, Wilaya ya Kigamboni.

MILCOM
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akisaini kiambu cha wageni, alipowasili kwenye Ofisi za Kampuni ya kuzalisha na kusindikaji maziwa na maji ya Milcom, wilayani Kigamboni. Kulia ni Mkurugnezi wa kampuni hiyo, Said Nahdi na kushoto ni Mkuu wa wilaya hiyo, Hashim Ngandirwa
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza
Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Said Nahdi akimtembeleza Makonda na msafara wake, katika maeneo mbalimbali ya kiwanda chake.

Makonda na msafara wake, wakipatiwa maelezo ya kitaalam katika usindikaji maji safi.
Makonda na msafara wake, wakipatiwa maelezo ya kitaalam katika usindikaji maji safi.
Mkurugenzi wa kampuni hiyo akiwapa maelezo Makonda na baadhi ya viongozi wengine
Msafara wa kukagua shughuli za kiwanda ukiendelea

USINDIKAJI MAZIWA
 
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akishuhudia maziwa yanavyotolewa kwenye ng'ombe moja kwa moja kwa ajili ya kusindikwa katika kiwanda hicho

Makonda akizungumza na waandishi kuhusu alichoshuhudia
Baada ya kukagua eneo la usindikaji maziwa 
ENEO LA USINDIKAJI
KAIMU MGANGA MKUU (DMO) KIGAMBONI ALIPONUSURIKA KUTUMBULIWA PEMBA MNAZI
Kaim Mganga Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, akiwa mtulivu wakati mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, akimuuliza maswali mbalimbali baada ya kubainika kwamba usimamizi wa zahanati yaTundwi, Pambamnazi, ulikuwa hauridhishi na hivyo kusababishwa wananchi kukosa huduma kwa kiwango kinachstahiki. Hata hivyo Makonda alimsamehe baada ya kujulishwa kuwa ameshika nafasi hiyo kwa mda mfupi. lakini akamtaka kuchapa kazi ili kuthibisha kuwa anafaa kuwa DMO kamili 
Wananchi Pemba Mnazi
Makonda akizindua ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa shule ya Pemba Mnazi
Mwanafunzi shule hiyo akisoma maelezo yaliyopo kwenye jiwe la msingi
Makonda akihitimisha ziara yake Pemba Mnazi kwa kuzungumza na wananchi. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO-CCM Blog +255 712 498008

No comments: