Kampuni Maarufu ya KAGOYA ya Nchini Japan Imeshambuliwa kimtandao ambapo taarifa binafsi na za kibenki za wateja wake zimedukuliwa.
Uhalifu huu umegundulika mwezi huu (Desemba, 2016) na tayari kampuni husika imesha toa taarifa kwenye vyombo vya usalama vya Nchini humo - Ambavyo pia vimeanza uchunguzi rasmi jana.
Kampuni hiyo imesema, Wateja wake waliotumia "Credit card " zao baina ya Aprili Mosi , 2015 hadi september 21, 2016 wameathiriwa na uhalifu huu na imewaasa wateja wake wafatilie taarifa za utoaji pesa wa kadi zao.
Taarifa binafsi takriban Elfu 50 pamoja na taarifa za kibenki takriban Elfu 21 zimeathirika katika shambulio hili la kimtandao.
Mjumuiko wa taarifa zilizo ibiwa ni, majina , barua pepe, Namba za simu, Namba za kadi za benki, maneno ya siri (Nywila) pamoja na taarifa nyingine za wateja wake.
Hii si mara ya kwanza kwa Nchi ya JAPANI kupata shambulio kubwa la kimtandao kwa mwaka huu (2016) pekee - Itakumbukwa, Mwezi May mwaka huu (2016) zaidi ya Yuan Bil. 1.5 sawa na Dola Milioni 13 ziliibiwa katika ATM zaidi ya 1400 ndani ya masaa mawili na nusu.
Aidha, TANZANIA hali ya uhalifu mtandao bado ni changamoto inayo hitaji suluhu ya kudumu. Kuibiwa kwa Fedha na Taarifa , Matumizi mabaya ya mitandao, Tovuti kudukuliwa ni miongoni mwa matukio yaliyo jitokeza kwa mwaka huu 2016.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (UUW) imeleza Waziri mwenye dhamana wa wizara hiyo ametaka kupatikana kwa mwarubaini wa wimbi la wizi mtandao unapatikana Nchini.
Akizungumza wakati wa uzinduzi Bodi ya TCRA (Mamlaka ya Mawasiliani Tanzania) Mheshimiwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa ameitaka Bodi mpya ya TCRA, kuhakikisha wanapata mwarobaini wa kudhibiti ongezeko la wizi wa mitandao unaoendelea kukithiri hapa nchini.
Prof. Mbarawa amesema watanzania wameibiwa kwa muda mrefu kupitia njia ya ujumbe mfupi na kushawishiwa kutoa fedha kwa njia ya udanganyifu na hivyo kuitaka bodi hiyo kutofumbia macho changamoto hiyo.
“Changamoto ya wizi wa mitandao inagusa watanzania wengi, mkiwa na jukumu la kudhibiti mna wajibu wa kuwalinda wananchi”, amesema Waziri Prof. Mbarawa.
Ameongeza kuwa bodi hiyo ihakikishe inasimamia kwa karibu sheria, kanuni na taratibu zilizowekwa katika kudhibiti ubora wa masuala ya mawasiliano ikiwa ni teknolojia inayokuwa kwa kasi kubwa.
Aidha Prof. Mbarawa ameitaka bodi hiyo kuendelea kudhibiti wimbi la meseji za uchozezi zinazotumwa na baadhi ya wananchi kwa kukosa maadili.
Katika kuimarisha huduma ya teknolojia ya habari na mawasiliano nchini Waziri Prof. Mbarawa ameikata TCRA kufanya maamuzi ya haraka na kuwa wabunifu ili kuweka mazingira endelevu ya kukuza sekta hiyo.
Aidha, Mwenyekiti wa Bodi mpya ya TCRA Dkt. Jones Kilimbe amesema kuwa pamoja na changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta hiyo, Bodi itahakikisha inapata suluhu ya changamoto hizo ndani ya muda mfupi.
Hatuna Budi kutambua kua janga la uhalifu mtandao ni kubwa na athari zake zimekua zikionekana situ kwa nchi zisizo na teknolojia nzuri ya kukabiliana na uhalifu mtao bali pia Nchi zilizo endelea zimekua wahanga wa janga hili.
Taifa la Tanzania halina budi bali kuanza na utayari uliombatana na kujipanga upya na vizuri kukabiliana na Wimbi la uhalifu mtandao nchini.
Changamoto za urasimu, matumizi makubwa ya pesa kwenye kampeni za kukuza uelewa zinazokosa matokeo chanya pamoja na kutojiongezea elimu ya mara kwa mara ya kukabiliana na uhalifu huu mtandao lazima ipaiwe suluhu.
Sheria Mtandao pekee haziwezi kutuvusha kwenye wimbi hili la ukuaji wa uhalifu mtandao nchini, Lazima mambo mengine muhimu ya kukabiliana na uhalifu mtandao yafanyiwe kazi.
Naziasa taasisi binasfi na za serikali kujenga tabia ya kutoa taarifa ya matukio ya kishambulizi mtandao mara tu yanapo gundulika ili iwe rahisi kupatiwa suluhu. Bila kufanya hivyo wahalifu mtandao wataendelea kupata nguvu.
Kwa sasa Tanzania, Hatujafikia pabaya sana kulinganisha na mataifa mengine – Ila, Kama hatua za haraka na za dhati za kujipanga na kufunga mikanda hazitachukuliwa mapema, Mbele yetu ni mbaya Mno.
Kumeonekana mapungufu makubwa maeneo mbali mbali Nchini ambayo yanaweza kupelekea taifa kutumbukia kwenye hali mbaya ya uhalifu mtandao ambapo taarifa na tafiti mbali mbali zinazo fanywa nchini na nje ya nchi zime baini mapungufu mabali mbali yanayoweza kupelekea wadukuzi kutuingiza matatizoni.
Ni wajibu sasa kufanyia kazi mapendekezo yanayo tolewa ili kujiweka salama kimtandao.
No comments:
Post a Comment