Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Aziz Mlima akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Tume ya Pamoja ya Kudumu ya Ushirikiano (JPC) kati ya Tanzania na Kenya uliofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam. Mkutano huo pamoja na mambo mengine utajadili maeneo mbalimbali ya ushirikiano ikiwemo sekta ya Elimu, Afya na Kilimo.
Balozi Ben Ogutu, Kiongozi wa Ujumbe wa Kenya akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano wa JPC kati ya Tanzania na Kenya
Mkurugenzi wa Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Samwel Shelukindo akizungumza wakati wa Mkutano wa JPC kati ya Tanzania na Kenya
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ambaye pia alikuwa mshereheshaji akizungumza, Bi. Mindi Kasiga.
Balozi wa Kenya hapa nchini, Mhe. Chirau Ali Mwakwere akifuatilia ufunguzi wa Mkutano wa Tume ya Pamoja ya Kudumu ya Ushirikiano kati ya Tanzania na Kenya
Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Kenya, Bi. Talha Mohammed (kulia) naye akifuatilia ufunguzi wa Mkutano wa JPC.
Sehemu ya wajumbe kutoka Kenya wakifuatilia ufunguzi wa Mkutano wa JPC
Sehemu nyingine ya wajumbe kutoka Tanzania wakifuatilia mkutano
No comments:
Post a Comment