Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Edwin Ngonyani (Kushoto), akifafanua jambo kwa Mbunge wa Jimbo la Mlimba Mhe. Suzani Kiwanga (Wa tatu kulia), wakati alipokagua barabara ya Ifakara, Taweta hadi Madeke (KM 225) Mkoani Morogoro.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Edwin Ngonyani (aliyenyoosha kidole), akizungumza na wananchi wa Mlimba wilaya ya Kilombero Mkoani Morogoro wakati alipokagua barabara ya Ifakara, Taweta hadi Madeke (KM 225)
Wanakijiji wa kata ya Msagati wilaya ya Kilombero Mkoa wa Morogoro wakicheza ngoma na Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Edwin Ngonyani baada ya kuhakikishiwa barabara ya Ifakara –Kihansi (KM 130) itajengwa kwa kiwango cha lami.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Edwin Ngonyani (Wa tatu kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Mbunge wa Mlimba Mhe. Suzani Kiwanga (Wa pili kushoto) kabla ya mkutano na wanakijiji wa Msagati Mkoani Morogoro.
Wanakijiji wa kata ya
Msagati wilaya ya Kilombero Mkoa wa Morogoro wakimsikiliza Naibu Waziri wa
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Edwin Ngonyani (hayupo pichani) wakati
wa mkutano na wanakijiji hao.
Picha na Wizara ya
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
Naibu Waziri wa
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Edwin Ngonyani ameutaka uongozi wa
Wakala wa Barabara nchini TANROADS Mkoa wa Morogoro kuhakikisha wanafanya
matengenezo katika barabara zao ili ziweze kupitika katika kipindi chote cha
mwaka.
Mhandisi Ngonyani
ameyasema hayo mara baada ya kukagua barabara ya Ifakara, Taweta hadi Madeke (KM
225) ambapo amesema barabara ya Ifakara –Kihansi (KM 130) imeshafanyiwa upembuzi yakinifu na usanifu wa kina unaendelea
ili kipindi cha miaka mitano iweze kujengwa kwa lami.
“Katika miaka hii
mitano tutahakikisha maandalizi ya awali ya kuwezesha barbara hii kujengwa kwa
kiwango cha cha lami yanakamilika na hivyo kutuwezesha kutenga fedha kwa ajili
ya kuanza ujenzi rasmi”. amesema Mhandisi Ngonyani.
Amesema kuwa barabara
hiyo ni kiungo muhimu kwa wakazi wa Ifakara na Kilombero kwa kuunganisha na
Mkoa wa Njombe na hivyo kukamilika kwake zitafungua fursa za kiuchumi na
kibiashara kwa wananchi hao.
Mhandisi Ngonyani
amesisitiza kuwa Serikali ya awamu ya
tano itaendelea kutekeleza ahadi zote zilizotolewa kwa wananchi kwa kuunganisha
mikoa mbalimbali kwa ujenzi wa barabara bora kwa viwango vya lami ili kurahisisha
usafiri na kuongeza kasi ya maendeleo kwa wananchi.
“Serikali ya awamu ya
tano ipo madarakani kwa ajili ya wananchi bila kujali itikadi zao,tumewahaidi
kuwaletea maendeleo hivyo tutajenga barabara zote tulizozihaidi kwa wakati ili
wananchi waendelee kunufaika na matunda ya serikali yao”.amesisitiza Mhandisi
Ngonyani.
Ameongeza kuwa
Serikali kupitia Wizara yake itaboresha huduma za mawasiliano katika shemu
mbalimbali za nchi ili kuwawezesha wananchi kuwasiliana wakati wowote ili
kukuza mahusiano yao kiuchumi, kibiashara na hivyo kukuza pato lao na la taifa.
“Tumeuomba uongozi wa
kila wilaya utuletee maeneo ambayo huduma za mawasiliano hazijafika au
zinasumbua ili sisi tuweze kuzishghulikia na kuzipatia huduma bora za
mawasiliano”. Amesistiza Mhandisi Ngonyani.
Naye Mbunge wa Jimbo
la Mlimba Mhe. Suzani Kiwanga ameishukuru Serikali kwa uamuzi wa kuiweka barabara hiyo katika mpango wa
kuijenga kwa kiwango cha lami kwa kuwa itafungua fursa mbalimbali kwa wananchi ambo
wataweza kusafirisha mazo yao kwenda katika masokoni kwa urahisi.
Naibu Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano yupo Mkoani
Morogoro katika ziara ya kukagua Miundombinu ya barabara, Madaraja na Reli.
Imetolewa
na kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano.
No comments:
Post a Comment