Tembea ujionee dunia imebebea mengi
Kila siku tupo mtaani siyo kwamba good life hatupendi
Sina mi nakaa, siwezagi kuji-pretend.
Sikati Tamaa (Darassa)
Siku inapoisha nashukuru kwa mwenyeji
Umri ungechagua ningesema hapa siongezi
Majukumu yanakua napunguza unyamwezi.
Sikati Tamaa (Darassa)
Kila siku labda kesho na kesho haitokei, kila kitu unachopanga hakielekei, mpaka unahisi labda Mungu kwako hajaweka better days.
Sikati Tamaa (Darassa)
Kweli dunia haiko-fear, mwanangu imemtokea, ye ni innocent man na anaozea Segerea, jembe lake halitumiki kama kitaa la Babu Seya, familia yake imemmisi na ina-wish atatoke.
Sikati Tamaa (Darassa)
Nyumbani kwenu wewe ndiyo mlezi na ulipaswa kulelewa
Umekabidhiwa jezi na mchezo haujauelewa.
Sikati Tamaa (Darassa)
Moyo wa ubinadamu kazi wengine mtanipendaga nikisepa
Too Much (Darassa)
Mwingine anakutafuta hana dili
Mwingine atakukuta tu umechili
Analeta maneno ya Kiswahili
Anataka kujua unalipaje bili.
Too Much (Darassa)
Wengine ndiyo washkaji
Ukigeuka mgongo ndiyo wauaji.
Too Much (Darassa)
Ukitaka kula bata uache kumchunguza
Aah! Kama utanipenda
Sitojali shida ulizobeba
Na kama unataka kucheza
Katafute refa wa kukubeba.
Kama Utanipenda (Darassa)
Jitazame kwenye kioo how beautiful you are
Mapenzi ukichaa, mapenzi uchizi
Uwe nacho ukikataa, mwingine inamnyima usingizi
Mwingine atakesha, mwingine atatesa
Mwingine atataka akutumie kama pesa.
Kama Utanipenda (Darassa)
Muziki (Darassa)
Wanaoota mapembe waongezee mkia
Na ukinibeep tu nakupigia.
Muziki (Darassa)
Blaa blaa sitaki kusikia
Siyo simba siyo chui siyo mamba ahh
Ngozi yangu inatosha kujigamba ahh
Na sina maneno ya kwenye kanga
Kazi juu ya kazi
Yani bamba tu bamba.
Muziki (Darassa)
Unataka kukimbia na hauna break
What do you expect?
Muziki (Darassa)
Maisha yetu ya kila siku kama vile movie
Vitu vingine havitakagi ujuaji
Utajikuta unatandikia watu jamvi
Kusubiria embe chini ya mnazi.
Muziki (Darassa)
Kumuelewesha chizi utajipa kazi
Funga mkanda kaza na kamba
Ama ufuate nyayo uchane msamba.
Muziki (Darassa)
Usifuge chuki maana haitakusaidia
Bora ufunge mbwa ataweza kukulindia
Dunia kubwa mtu mmoja hawezi kujaa dunia.
Tunaishi (Darassa)
Enjoy ulichopewa, Mungu atakuongeza
Maisha ni kujiamini
Wakikuuliza unataka kuwa nana sema ‘mimi’.
Sio Mbaya (Darassa)
Sina mistari ya majungu kikuchana nakutagi.
Kaa Tayari (Darassa)
Boss kamganda Dangote kaisahau Tip Top.
Kaa Tayari (Roma)
Bungeni sioni kinachoendelea
Naona wasomi wakisutana umbeya
Wengine walishikwa ugoni picha zilienea
Hamuwaoni jimboni afu bado mnawalea.
Viva Roma (Roma)
Show zangu baunsa anacheza
Mchecheto ulimpata Jaguar
We nianzishe kwenye show nisepe na kijiji.
K.K.K (Roma)
Wanatugawa kimakundi watumeze
Ona anakonda famili lahi wallah
Leo Jide anamjua Songa.
K.K.K (Roma)
Wadau wana chenga nyingi kama walichezea
Tukuyu
Na kufumba macho siyo njia ya kuikwepa ngumi
ya uso.
K.K.K (Roma)
Nilipotoka ni mbali enzi nadandia mafuso
Unaweza sali uzae chema ukazaa shoga na
msagaji
Mpagani akabakwa ikatunga mimba akamzaa
padri.
K.K.K (Roma)
Aliyepata ziro form four
Mnamsukuma aende Veta
Mnaamini umeme wa magari ndiyo unahitaji
mazezeta!
2030 (Roma)
Mzee wa bandari kastaafu kajenga banda la uani
Ana wake wa tatu, je watoto watarithi nini?
Ndo chanzo cha kurogana na kutupiana majini
Huyu akimpandisha Makata, yule Maimuna Subian.
2030 (Roma)
Pesa ilileta ubaguzi kati ya Loyola na Pugu
Pesa ndo ilichochea beef ya Nice na Dudu
Na pesa ndo ilimaliza vita ya Ruge na Sugu.
2030 (Roma)
Waziri anaziuza pembe za ndovu na meno ya tembo
Nchi imejaa misitu tuna uhaba wa madawati
Tunakula vitu feki TBS mko wapi?
2030 (Roma)
Amana wanatelekeza watoto wanalia Mwananyamala
Wanatuua na hawaendi jela, jela anakwenda Kajala.
2030 (Roma)
Ndoto zangu kitambo zilikuwa niwe padre
zikayeyuka nilipopuliziwa moshi wa widi!
Mathematics (Roma)
Bado nawaza Diva angekuwa mchepuko wa Mengi
Ayaa ya ya ya we mama yangu, tungeona mengi.
Una Akili Wewe (Roma)

No comments:
Post a Comment