ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, December 21, 2016

MKE AMPA KICHAPO MUMEWE HADHARANI MOSHI

Mwanamke mmoja anayefahamika kwa jina la Mama Tundu amempa mumewe kichapo na kumjeruhi usoni akimtuhumu kutoacha matumizi ya nyumbani.
Tukio hilo lililovuta umati wa watu lililitokea jana saa 2:00 asubuhi mtaa wa Msaranga Wilaya ya Moshi, baada ya mwanamke huyo kumtuhumu mumewe, Fredrick Masawe kutotoa fedha za matumizi.
”Nimechoka na tabia yake ya kunywa pombe kila wakati wakati sisi tunalala njaa kisa eti fedha zote anatumia baa na wanawake wake, siwezi vumilia leo mpaka kieleweke,'' alidai mwanamke huyo.
Akizungumza na gazeti hili baada ya kuamuliwa, mumewe alikanusha kuwa na wanawake bali mara nyingi huwa na marafiki wanaofanya kazi pamoja na kwamba pombe hizo hununuliwa na marafiki zake.

Chanzo: Mwananchi

2 comments:

Anonymous said...

Tuwekee walau tupicha tuwili tuone ukweli wenyewe. Kauli tu hatuelewi. Si ndio kusomeka kwa namba? Na bado sikukuu na mwaka mpya ikifuatiwa na kufunguliwa mwaka wa shule! Kitaeleweka tuuh. Habari ya mjini kaburi la faru John kitendawili!!

Anonymous said...

na apigwe tu maana hakuna namna/jinsi.mfumo dume uzembe uzembe huu na ufee.piga piga mama.