Advertisements

Thursday, December 1, 2016

MOBISOL NA ZUKU TV WAZINDUA HUDUMA ZA TELEVISHENI YA SATELITE YA NISHATI YA JUA

Meneja Mkuu wa Zuku Tv Tanzania , Bw.Omari Zuberi akiongea na waandishi wa habari juu ya huduma mpya ya TV ya nishati ya jua ambayo ina channel za Zuku Tv 
katikati ni Afisa masoko wa Mobisol Sjors Martens akiwa na wafanyakazi wa mobiso l katika uzinduzi huo hii leo jijini Arusha
mmoja wa mmteja wa mobisol ambaye akutaka kutaja jina lake akiongea wakati wa uzinduzia ambapo aliisifia kampuni ya mobisol nakusema ni mtetezi wa wananchi wanaoishi vijijini ambapo umeme haujafika
Meneja wa zuku Tanzania wa kwanza kushoto akibadilishana mawazo na wa kwanza kulia ni afisa usiano wa Zuku dada Yasta pamoja na mwakilishi wa zuku Jack Karanja katika uzinduzi 
wafanyakazi wa zuku wakifurahia mara baada ya uzinduzi 
Na Woinde Shizza,Arusha


KAMPUNI inayoongoza kwa utowaji wa huduma za nishati ya jua majumbani ,Mobisol na Kampuni ya Zuku Tv inayotoa burudani za satellite wameungana pamoja kwa ajili kuwanufaisha watanzania wasiounganishwa na nishati ya umeme.

Kwa pamoja kampuni hizi zimezindua kwa mara ya kwanza TV ya nishati ya jua ambayo ina channel za Zuku Tv huduma inayowalenga wale ambao hawajafikiwa na umeme wa gridi ya Taifa.

Huduma hii huunganisha mfumo wa nishati jua, televisheni ya hadi inchi 32 ya nishati jua, ungo wa satellite, na huduma ya ya kifurushi cha Zuku Smart Plus chenye chanelli 47 and 18 za redio. Mobisol wanalenga kutoa huduma hii kwa watanzania ambao hawajafikiwa na huduma ya nishati ya umeme, kwa kutoa nashati safi na ya kuaminika kwa bei nafuu popote ulipo katika mfumo moja mkamilifu.

Mobisol inatoa vifurushi mbalimbali vya nishati ya jua ya majumbani, vilivyo na uwezo wa kutoa nguvu ya umeme hadi 200W, unaotosha matumizi ya kaya nzima. Kila kifurushi kintaota paneli ya PV, betri ya nishati ya jua, taa nne za mwanga mkali,TV kubwa ya kioo cha bapa, tochi, chagi ya simu na redio ambayo unaweza kuichagi. Vifaa hivi vinapatikana na waranti, huduma ya kufungiwa bure, huduma ya wateja na huduma ya marekebisho kwa miaka 3. Pia, Kwa kuongezaTsh 8,999 kwamwezikwakifurushi, watejawatawezakupatahudumazaZuku TV kwamudawamasaasabakwasiku .

Akizungumza katika uzinduzi huo Afisa masoko wa Mobisol Sjors Martens alisema kuwa wao wanania ya kuleta maisha mazuri kwa wateja wao nchini Tanzania.

Alisema Huduma yao ya kifurushi cha televisheni ya satellite kitawezesha wateja kufurahia habari , michezo, burudani na maudhui ya elimu wakati wowote hata wakiwa wanaishi mjini au vijijini.

Kwa upande wake Meneja Mkuu wa Zuku Tv Tanzania , Bw.Omari Zuberi alisema ubunifu wa huduma hii itatuwezesha  kufikia zaidi ya watanzania million 8 ambao hawajawa na nishati ya umeme wa grid ya Taifa na kutuwezesha kuchangia kwa asilimia kubwa ongezeko la televesheni nchini.

“Hii ni fursa ya kipekee na ya kuleta hamasa kwa wateja wa Mobisol kuwa na uwanja mpana zaidi wa kuchagua na kufurahia zaidi ya chaneli 40 za Zuku TV inayotambulika kama huduma bora ya bei nafuu inayotoa burudani kwa familia kwa kuhamasisha maudhui ya kinyumbani zaidi,” alisema Zuberi.

Aliongeza kuwa Ingawa asilimia 70 ya watanzania hawajafikiwa na huduma ya nishati ya umeme na asilimia kubwa ya watanzania bado hawana Televisheni, Mobisol na Zuku wametumia fursa hii na kuungana pamoja kwa ajili ya kutoa huduma ya umeme wa jua na kutoa burudani ya TV Satellite yenye ubora wa kimataifa

Aidha alisema kuwa Huduma hii ya PayTV iliozinduliwa mkoani hapa itapatikana katika mikoa ambayo Mobisol inatoa huduma ambapo ni Arusha, Manyara, Kilimanjaro, Tanga, Pwani, Singida, Tabora, Dodoma, Mwanza, Shinyanga, Geita, Mara, Kagera, Simiyu, Mbeya, Songwe na Njombe - na baadaye kote nchini mwaka ujao

Alibainisha kuwa Kupitia Zuku TV, watanzania wanaweza kufurahia idadi ya channel za kusisimua ikiwa ni pamoja na channel za nyumbani FTA, channel za kimataifa na channel za Zuku asili; Zuku Sports, hivi karibuni ilizindua tena Zuku Swahili, Zuku Kids, Zuku Life Glam na Zuku Nolly.

Alisema kuwa Bei ya kifurishi cha Zuku smart pack kitakuwa kikiongezwa kwa awamu katika mfumo nishati ya jua ya Mobisol, ambayo wateja hulipa kupitia simu kwa kipindi cha miaka mitatu.

Alifafanua kuwa Baada ya miaka mitatu, wateja watamili hivyo vifaa na kupata ofa ya kuvutia kwa kulipa tena huduma hiyo mpya

No comments: