ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, December 6, 2016

SALAMU ZA RAMBI RAMBI - KIFO CHA PROF. MTULIA

Image result for chama cha mapinduzi
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Kanali mstaafu Abdulrahman Kinana amemtumia salamu za rambi rambi Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Pwani Ndg. Mwishehe Shaban Mlao kufuatia kifo cha Profesa Idrissa Ali Mtulia, Mbunge mstaafu wa Jimbo la Rufiji kilichotokea jana tarehe 05 Desemba, 2016 jijini Dar es salaam.

Prof Mtulia ameshika nyadhifa mbalimbali za uongozi na utumishi katika Chama na Serikali. Alikuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), Mbunge wa Jimbo la Rufiji, Katibu Mkuu wizara mbalimbali, Daktari wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Awamu ya Pili na Mwenyekiti wa Bodi ya Madawa (MSD)

Prof Mtulia, atakumbukwa na wanachama wa CCM na Wananchi wa Mkoa wa Pwani kwa jitihada zake za ujenzi na uimarishaji wa Chama na mchango wake mkubwa katika maendeleo ya Wananchi wa Rufiji.

Hakika sisi ni wa MwenyeziMungu na kwake yeye ndio marejeo yetu. 

Imetolewa na:-
                   
Christopher Ole Sendeka (MNEC)
MSEMAJI WA CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)
06.12.2016

No comments: