ANGALIA LIVE NEWS

Friday, December 30, 2016

SHUKURANI ZA DHATI KUTOKA FAMILIA YA MKANDE

Familia ya Michael na Grace Mnkande pamoja na jamaa yote ya Mnkande na Hiza walioko Marekani na Tanzania. Wanapenda kutoa shukrani zao za dhati kwa ndugu,jamaa na marafiki wote, mliotumia muda wenu, hali na mali zenu, na hata maombi yenu katika kipindi kigumu na kizito kwetu cha msiba wa kuondokewa na mama yetu mpenzi ROSE SHEDAFFA MNKANDE.

 Upendo wenu umedhihirika kwetu pale ambapo mlilipokea jambo hili kama la kwenu, bila kujali baridi kali, mliweza kufika kutufariji na kutupa misaada mbalimbali kama tulivyoeleza hapo juu.
Si rahisi kutaja mtu mmoja mmoja ila tunawaomba mpokee shukurani zetu toka vilindi vya mioyo yetu. 

Mwenyezi Mungu awabariki kila mmoja wenu awazidishie pale mlipopunguza kwa ajili yetu. Nasi twawatakia amani, furaha, upendo na mafanikio mema kwa mwaka mpya,2017. Mungu awabariki.

No comments: