ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, December 4, 2016

TFF yazibariki Yanga na Azam michuano ya Afrika

 Shirikisho la Soka nchini TFF limetoa leseni ya awali kwa vilabu vya Yanga na Azam FC ambazo zinashiriki mashindano ya kimataifa hapo mwakani.

Afisa habari wa TFF Alfred Lucas amesema, leseni hiyo ni uthibitisho kuwa wana vigezo vyote vinavyowafanya kushiriki michuano ya ligi kuu pamoja na mashindano ya kimataifa.

Vigezo hivyo ni pamoja na umiliki wa klabu wa mtu mmoja, uwanja wa nyumbani wa kuchezea, uwanja wa kufanyia mazoezi na timu ya vijana ambayo inapata huduma zote ikiwemo matibabu pamoja na ushiriki wake katika mashindano mbalimbali ya vijana.

Alfred amesema, leseni hiyo imetoka mara baada ya vilabu hivyo kujaza fomu ambazo zinaonyesha wachezaji pamoja na benchi la ufundi litakalotumika katika mashindano ya kimataifa na jana ilikuwa mwisho kuwasilisha fomu ambapo Yanga itashiriki mashindano ya Klabu bingwa Afrika huku Azam FC ikishiriki Kombe la Shikisho Afrika.
Iwapo klabu mojawapo au zote zitakuwa na mabadiliko kati ya wachezaji au kocha zitalazimika kulipia faini ili kuongeza au kufanya marekebisho ya aina yoyote.


Alfred amesema, mara baada ya kupata leseni hiyo Shirikisho la Soka barani Afrika CAF watakuja kwa ajili ya kufanya uthibitisho ambao utasaidia vilabu hivyo kupata leseni ya CAF na watakuwa katika maandalizi huku wakisubiri kupangwa kwa ratiba ya mashindano yanayotarajiwa kuanza kutimua vumbi mapema mwakani.

No comments: