ANGALIA LIVE NEWS

Friday, December 30, 2016

WAKWEPA KODI WA ARDHI NA MAJENGO HADHARANI WIKI IJAYO

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi amesema kwamba kuanzia wiki ijayo wizara yake itawatangaza hadharani watu wote ambao wamekwepa kulipa kodi ya ardhi na majengo, wakiwemo vigogo walioko serikalini.

Akifungua semina juu ya jukumu la vyombo vya habari katika kutoa elimu ya sheria, kanuni na taratibu katika utawala wa ardhi ili kusaidia kutatua migogoro, iliyofanyika mjini Morogoro, Lukuvi alisema kwamba watayatangaza majina hayo ili watu wawajue watu wanaojenga majumba ya kifahari lakini hawataki kulipa kodi ya serikali.
“Tutatangaza majina yao halisi sio yale ya bandia, ili watu wawajue kuwa kuna watu wamejenga majumba ya fahari, lakini hawalipi kodi ya serikali, baada ya kutangaza tutawapiga faini. Na mwakani tutaweka kodi kubwa zaidi kwa mashamba na viwanja visivyoendelezwa,” alisema Lukuvi.
Aidha Waziri Lukuvi alisema hata hivyo kwa sasa upigaji umepungua wizarani kwake “Hakuna siri, wizi hakuna,
ujambazi, rushwa zimepungua sana, mtu akiniambia ameombwa rushwa pale wizarani nitamshangaa, tunataka iwe wizara salama inayotoa hati kwa haraka,” alisema. Miaka 10 nchi yote iwe imepangwa, kupitia kanda nane ili kuepusha watu wote kwenda makao makuu ya wizara kwa ajili ya kufuatilia hati kusajiliwa.”

CHANZO: HABARILEO

No comments: