Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Eng. Joseph Nyamhanga akitoa maelezo kwa Wadau wa masuala ya Ujenzi katika hafla ya uzinduzi rasmi wa mwongozo wa kuimarisha ushirikishwaji wa wanawake katika kazi za barabara uliofanyika katika ukumbi wa makumbusho ya taifa jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Eng. Joseph Nyamhanga akitoa maelezo kwa katika Wadau wa masuala ya Ujenzi katika hafla ya uzinduzi rasmi wa mwongozo wa kuimarisha ushirikishwaji wa wananwake katika kazi za barabara uliofanyika katika ukumbi wa makumbusho ya taifa jijini Dar es salaam.
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi) Eng. Joseph Nyamhanga (kulia) akizindua kitabu cha mwongozo wa kuimarisha ushirikishwaji wa wanawake katika kazi za barabara uliofanyika katika ukumbi wa makumbusho ya taifa jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Eng. Joseph Nyamhanga (kulia) akizindua kitabu cha mwongozo wa kuimarisha ushirikishwaji wa wanawake katika kazi za barabara uliofanyika katika ukumbi wa makumbusho ya taifa jijini Dar es salaam.
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi) Eng. Joseph Nyamhanga (kulia) akizindua kitabu cha mwongozo wa kuimarisha ushirikihwaji wa wanawake katika kazi za barabara uliofanyika katika ukumbi wa makumbusho jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi wa barabara Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng Ven Ndyamkama akifafanua jambo kwa waandishi wa habari kuhusu mwongozo wa kuimarisha ushirikishwaji wa wanawake katika kazi za barabara,jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Wizara ya
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi) Eng. Joseph Nyamhanga katika
picha ya pamoja na wajumbe wa maendeleo ya sekta ya ujenzi mara baada ya
kuzindua kitabu cha mwongozo wa kuimarisha ushirikishwaji wa wanawake katika
kazi za barabara uliofanyika katika ukumbi wa makumbusho ya taifa jijini Dar es salaam. Picha na Wizara
Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
Imeelezwa kuwa sababu
za kihistoria, mila na desturi za jamii ni moja ya changamoto zinazoikabili
sekta ya ujenzi kwenye ushirikishaji wa wanawake katika utekelezaji wa miradi
ya barabara nchini.
Kauli hiyo imetolewa
na Katibu Mkuu wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano (sekta ya ujenzi ),Eng.
Joseph Nyamhanga wakati akizindua mwongozo wa kuimarisha ushirikishwaji wa
wanawake katika kazi za barabara ambapo Serikali imekuja na mikakati mbalimbali
ya kuwashirikisha wanawake katika miradi ya ujenzi wa barabara
"Maandalizi ya
mwongozo huu ni sehemu ya mkakati wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
katika utekelezaji wa mikakati mbalimbali iliyojiwekea ili kuinua maisha ya
wanawake kiuchumi,'' amesema Eng. Nyamhanga.
Eng. Nyamhanga
ameongeza kuwa utekelezwaji wa mwongozo huo ni moja ya kichocheo cha
kuwawezesha wanawake kutoa mchango mkubwa zaidi kuchumi nchini ambapo kwa sasa
sekta ya ujenzi inachangia asilimia 13.6 kwenye pato la Taifa.
Aidha ametanabaisha
kuwa kwa mwaka 2014/15 kumekuwa na ongezeko la ushiriki wa wanawake katika miradi
ya barabara wa uwiano wa kila wahandisi 100 wanaume wanawake 6 ambao kwenye
usimamizi wa miradi uwiano ukiwa ni asilimia 6.
Kwa upande wake
MKurugenzi wa Idara ya Barabara, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano,
Sekta ya Ujenzi, Eng. Ven Ndyamukama amesema ushirikishwaji wa wanawake katika
sekta ya ujenzi ulianza mwaka 1992 kwa
kutekelezwa kwenye mikoa ya Mbeya, Tanga, Shinyanga, Mwanza na Mtwara.
"Kama Wizara
tuliona umuhimu wa kuanzisha kitengo maalum kwa ajili ya kuhakikisha
tunawawezesha wanawake katika kazi za ujenzi na hili limesisitizwa hata kwenye sheria
ya Ujenzi ya mwaka 2003 (CIP, 2003) kwa kuhakikisha wanawake wanashirikishwa
katika kazi za ujenzi ili kuwainua kiuchumi' amesema Eng. Ndyamukama.
Ameongeza kuwa pamoja
na mwongozo huu Wizara imeendelea kuwawezesha wanawake kwenye mafunzo
mbalimbali ya ujenzi kupitia vyuo mbalimbali vilivyo chini ya wizara na taasisi
binafsi.
Takwimu Kutoka Bodi ya
Usajili wa Wahandisi nchini (ERB) na Bodi ya Usajili wa Makandarasi (CRB) zinaonesha
kwa mwaka 2014, kati ya jumla ya wahandisi 13,148 waliopo nchini wahandisi
wanawake ni 926 ambao ni sawa na asilimia 6.5 wakati kati ya Makampuni ya makandarasi
8,071 yaliyosajiliwa ni makampuni 253 yanamilikiwa na wanawake sawa na asilimia
3.
No comments:
Post a Comment