Advertisements

Monday, January 16, 2017

Flora Mbasha Achumbiwa

STORI: MWANDISHI WETU, IJUMAA WIKIENDA
DAR ES SALAAM: Siku chache baada ya kutinga mahakamani kudai talaka kwa mumewe, Emmanuel Mbasha, staa wa Gospo Bongo, Flora Mbasha anadaiwa kuchumbiwa na mwanaume aliyetajwa kuwa ni mwenyeji wa Kahama, Sinyanga, Daud. Chanzo cha kuaminika kimepenyeza ubuyu wa motomoto kuwa, tukio la Flora kuvishwa pete ya uchumba lilijiri hivi karibuni baada mwanamuziki huyo wa Injili kutofautiana na ‘mlinzi’ wake aitwaye Peter Shelembi.
“Si unakumbuka baada yankutofautiana na Mbasha, Flora alikuwa ‘close’ na jamaa f’lani hivi anaitwa Peter, alikuwa akizurura naye sehemu mbalimbali kwa ajili ya kuwa kama mlinzi wake, akihofia Emma (Mbasha) anaweza kumletea fujo? Sasa nasikia mama’ke Flora alimshawishi bintiye aolewe na Daud, naye bila hiyana akakubali.

“Ilikuwa rahisi maana hata pale kanisani kwa Josephat Gwajima (Kanisa la Ufufuo na Uzima) alipokuwa anaabudu Flora alishaasi. Akaenda zake kuvishwa pete ya uchumba bila hata waumini wenzake kujua,” kilidai chanzo hicho. Baada ya kuzipata ‘good news’ hizo, Wikienda lilianza kwa kumtafuta Daud ili kumpongeza kwa kupata ‘kifaa’ na pia kujua mipango ya harusi. Tofauti na matarajio ya Wikienda
 kwamba pengine atazipokea pongezi na kumshukuru Mungu kuianza safari ya ndoa, jamaa huyo alipokea simu, baada ya mwandishi kujitambulisha, alikata. Wikienda lilipiga tena ili kutaka kujiridhisha labda pengine simu ilikatika kwa bahati mbaya lakini safari hii alipokea na kusema yeye si Daud, mwandishi amekosea namba, akakata tena simu.
Licha ya kujiridhisha namba hizo zinamilikiwa na Daud, Wikienda likaona isiwe kesi, likamvutia waya Flora ili kumpongeza na kumsikia anazungumziaje safari yake hiyo mpya anayoianza mbali na ile ya Mbasha iliyotawaliwa na ‘sarakasi’ nyingi hadi kufikia hatua ya kuishi kama paka na panya.
Baada ya Wikienda kujitambulisha na kumpongeza kisha kumpa ‘full mchapo’ kutoka kwa chanzo, Flora hakutaka hata kuzipokea pongezi hizo badala yake alisema hataki kuzungumzia jambo hilo na kushauri gazeti
hili lizungumze na mwanasheria wake.
“Jamani mimi sipo tayari kuzungumzia chochote zaidizaidi kama mnataka niwape namba ya mwanasheria wangu,” alisema Flora.
Flora alimtumia mwandishi wetu namba ya mtu aliyedai ni mwanasheria wake lakini alipopigiwa simu alisema kuwa, kuna kazi anafanya, apigiwe baada ya muda. Hata hivyo, baadaye simu yake ilipopigwa, haikupatikana hewani. Flora aliishi kwenye ndoa na Mbasha kwa zaidi ya miaka kumi na kufanikiwa kupata mtoto mmoja, Elizabeth kisha mwaka 2015 walitengana kutokana na ugomvi wao uliofukuta chini kwa chini kwa muda mrefu na kuibuka hadharani baada ya Mbasha kupata msala wa kudaiwa kumbaka mdogo wa Flora. Hata hivyo, kesi iliunguruma kwa muda na baadaye Mbasha alishinda na kuachiwa huru.
GPL

No comments: