ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, January 18, 2017

KAMANDA RAS MAKUNJA AHOJIWA NA RADIO BBC KISWAHILI

Dar es salaam,
Kiongozi wa bendi maarufu Ngoma Africa aka FFU-Ughaibuni yenye makao nchini ujerumani mwanamuziki Ebrahim Makunja almaarufu Kamanda Ras Makunja mapema tu alihojiwa na radio BBC Kiswahili katika kituo chao Mikocheni jijini Dar,akiongoza mahojiano hayo mtangazaji Omari Mkambala
alimlima maswali Ras Makunja,katika moja ya majibu yake mwanamuziki huyo alisisitiza na kutoa wito kwa watanzania walio nje ya nchi kuwa mstari wa mbele kwa kuwapa ushirikiano bendi na wanamuziki wa Tanzania pale wanapoziona fulsa za kimataifa ii muziki wa Tanzania ufike nje ya mipaka na kupata soko zaidi la kimataifa,Kamanda Ras Makunja alisema muziki wa dansi na mengineyo ya kitanzania ina nafasi nzuri nje ya nchi kama watanzania wenyewe walio nje wakatakuwa na uzalendo wa kuwazipigania

bendi za nyumbani kutumbuiza katika majukwaa kimataifa. msikose kusikiliza mahojiano hayo katika radio BBC idhaa ya Kiswahili.

No comments: