ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, January 31, 2017

LEO NI MIAKA 7 YA BLOG YA VIJIMAMBO (HAPPY 7TH ANNIVERSARY VIJIMAMBO BLOG )

Image result for vijimambo logo
Kwanza tumshukuru Mwenyezi Mungu kwa rehema zake na leo Januari 31, 2017 ni siku iliyoanzishwa Vijimambo Blog miaka 7 iliyopita na kuzinduliwa tarehe 23 Oktoba 2010 na aliyekua Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Mwaanaidi Maajar katika ukumbi wa Mirage uliopo Langley Park Maryland.

Vijimambo Blog ni Blog isiofungamana na upande wowote ilianzishwa kwa lengo la kupashana habari na kuwa daraja na kiunganisho cha Diaspora na nyumbani Tanzania, kudumisha umoja wa Watanzania Diaspora hususani nchini Marekani. Vijimambo Blog ni blog mali ya WaTanzania, nayotumiwa na WaTanzania kwa lengo la kutoa taarifa mbalimbali zikiwemo habari zilizotokea muda huo, burudani na michezo, misiba, mahojiano na wadau mbalimbali wanaofanya vizuri popote Duniani na kuwa karibu na jamii inayotuzunguka.

Shukurani nyingi kwa wadau wote na mashabiki wa Vijiambo kwani bila nyinyi Vijimambo isingekuwepo hapa ilipo, shukrani za pekee kwa wadau wanaotangaza na Vijimambo Blog tunashukuru sana kwa kutuamini. Pamoja Blog shukurani nyingi sana kwa ukaribu wako na Vijimambo bila wewe tusingefikia hapa tulipo

Shukurani nyingi kwa timu nzima ya Vijimambo Tanzania, New York, Massachusetts, Houston, Texas Atlanta, Georgia, California, Columbus, Ohio na DMV wakiwemo wadau wa Vijimambo wanaotutumia habari zao bila kusahau Blog zote zinazoshirikiana kwa karibu na Vijimambo Blog ikiwemo TBN.

Shukrani za dhati kwa Dj Luke, Mubelwa Bandio, NY Eibra,  Kaley Pandukizi, Geofrey Adroph, Jojo, IskaJojo, Tembaphotos, Cassius Mpambamaji, Saleh Mohammed, Aloyce Mbullu, Willy, Baraka, Rachel Udoba, Amin Dola aka Mayor wa Seattle na Walter Minja Alex Kassuwi wakiwemo DICOTA USA bila kuwasahau Kamati ya Vijiamambo, Baraka Daudi, Asha Nyang'anyi, Idd Sandaly, Julius Katanga, Mayor Mlima, Asha Hariz, Tumaini Kaisi, Sunday Shomari na Mabare Matinyi

Shukurani za pekee kwa Ubalozi wetu wa Tanzania nchini Marekani na Mexico na Tanzania Mission New York kwa mashirikiano ya karibu, Ikulu, Ofisi ya Makamu wa Rais, Ofisi ya Waziri Mkuu, Wizara yetu ya mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Wizara ya mambo ya ndani, Idara ya Maelezo, Habari Leo, Mwananchi bila kusahau mashirika ya umma na binafsi na idara mbalimbali za serikali bila kuwasahau wasanii wote wanaotumia blog ya Vijimambo kwa kujitangaza.

Blog si jambo dogo ni kazi ya wito kama ilivyo udaktari na kazi ya kichungaji au aina yeyote ya kazi, inahitaji uvumilivu kwani inamaudhi mengi na kukatisha tamaa lakini siku zote hatusahau "MAFANIKIO NI MAPAMBANO NA MAENDELEO HAYAJI KWA KULALA" ndio maana pamoja na hayo yote timu ya nzima ya Vijimambo bado inaendelea kupambana mpaka kieleweke.

Tunawashukuruni mno wadau wote Blog yetu pedwa wa nnje ya Marekani na ndani. Na kama kuna yeyote tutakaekua tumemsahau naomba atuwie radhi kwani si kusudio letu kufanya hivyo.

Mwaisho sasa safari nyingine imeanza ya kuutafuta mwaka wa 8.
 Asanteni sana.

1 comment:

LINGA BOY. said...

Good job admin.. and your team,shukran ziwafikie wanavijimambo wote kwa news you're providing to wana diaspora,
Mambo mengi ya nyumbani tunayapata kupitia blog hii ya vijimambo kwa haraka na ufasaa zaidi , again asante sana kwa kazi nzuri mnayoifanya, Mungu hazidi kuidumisha blog ya vijimambo.