Advertisements

Monday, January 16, 2017

MAAFISA TEHAMA WA MAHAKAMA YA TANZANIA WAPEWA DARASA

 Mtendaji Mkuu Mahakama ya Tanzania, Bw. Hussein Kattanga  akifungua mafunzo Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA)  kwa Maafisa  TEHAMA   kutoka Mahakama  Kuu  ya Tanzania . Mafunzo  hayo ni ya  muda wa wiki moja yenye lengo la kuongeza ujuzi  yameanza leo katika  jengo  la  Shule ya Sheria lililopo Sinza, Kijitonyama jijini Dares Salaam na yanafanywa  na Mahakama  ya Tanzania kwa ushirikiano wa Wakala ya Serikali Mtandao(EgA).
 Mtendaji Mkuu Mahakama ya Tanzania, Bw. Hussein Kattanga  akifundisha  wakati akifungua  mafunzo Teknolojia ya Habari na Mawasiliano(TEHAMA)  ya  muda wa wiki moja yaliyoanza leo katika  jengo  la  Shule ya Sheria lililopo Sinza, Kijitonyama jijini Dares Salaam. Mafunzo hayo yenye lengo la kuongeza ujuzi  yanafanywa kwa ushirikiano wa  Mahakama ya Tanzania  na Wakala ya Serikali Mtandao(EgA).
Baadhi ya Maafisa  Teknolojia ya Habari na Mawasiliano(TEHAMA)  wakiwa katika   mafunzo ya muda wa wiki moja kuhusu kuwajengea uwezo  na ujuzi kwenye  masuala  ya TEHAMA yaliyoanza leo katika  jengo  la  Shule ya Sheria lililopo Sinza, Kijitonyama jijini Dares Salaam. Mafunzo hayo yanafanywa kwa ushirikiano wa wa  Mahakama ya Tanzania  na Wakala ya Serikali Mtandao(EgA).
  Mtendaji Mkuu kutoka Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora, Wakala wa Serikali Mtandao, Dkt. Jabir Bakari akitoa mada juu ya Serikali Mtandao wakati  wa mafunzo ya  Maafisa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano(TEHAMA) kutoka Mahakama Kuu ya Tanzania.Mafunzo hayo ni   ya  muda wa wiki moja yameanza leo katika  jengo  la  Shule ya Sheria lililopo Sinza, Kijitonyama jijini Dares Salaam na  yanafanywa kwa ushirikiano wa Mahakama  na Tanzania Wakala ya Serikali Mtandao(EgA).(PICHA NA MARY GWERA)

Mtendaji Mkuu Mahakama ya Tanzania, Bw. Hussein Kattanga amewataka Maafisa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano(TEHAMA) wa Mahakama ya Tanzania kutumia elimu na ujuzi  ili kuweza kutatua changamoto zilizopo kwenye masuala ya TEHAMA.
Kauli hiyo imetolewa na Mtendaji huyo wakati akifungua mafunzo hayo ya  muda wa wiki moja yaliyoanza leo katika  jengo  la  Shule ya Sheria lililopo Sinza, Kijitonyama jijini Dar es Salaam,  ambayo yanafanywa kwa ushirikiano wa  Mahakama ya Tanzania na Wakala ya Serikali Mtandao(EgA).
“Mnatakiwa kutumia elimu mliyonayo , ujuzi mtakaoupata  ikiwemo kuwa wabunifu katika  vitu vipya  ili kuweza kutatua changamoto zilizopo katika mifumo ya TEHAMA, alisema Mtendaji Mkuu, Bw. Kattanga.
Aliongeza kuwa maafisa hao wanatakiwa kufanya kazi kwa ushirikiano ili kuwezesha kufanya kazi  kwa ufanisi na kuleta matokeo chanya kwa pamoja kwenye shughuli za mifumo ya TEHAMA. Pia aliwataka kutumia ujuzi watakaoupata kuwafundisha wengine.
Bw. Kattanga aliwataka maafisa hao kuwa na uweledi katika  ya masuala ya Serikali Mtandao,  kujituma kufanya kazi  na kuacha tabia ya kulalamika ,ikiwemo  kuwa na mtandao wa kubadilishana mawazo katika masuala ya kitaaluma.
Akitoa mada kuhusu  Shughuli za Wakala ya Serikali  Mtandao, Bw. Bakari alisema  dhima yake ni  kusogeza huduma za Serikali kwa  wananchi kupitia dirisha moja, ili kuwezesha utendaji wa shughuli hizo  kwa gharama  nafuu , ubora , wakati na kuboresha ukusanyaji wa mapato ya Serikali.
 Alisema mfumo huo  pia  unasaidia kuboresha huduma za Serikali katika jamii.
Mafunzo hayo yamehusisha maafisa TEHAMA 25 kutoka katika kanda zote za Mahakama ya Tanzania.

No comments: