ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, January 7, 2017

Masjid Qadriya iliopo Buza Dar er Salaam inahitaji kisima

Assalamu aleikum ndugu zangu katika Imaan Naomba kuwataarifu kuwa Masjid Qadriya iliopo Buza Dar er Salaam inahitaji kisima ili waumini waweze kupata maji kwa ajili ya udhuu wakati wa Ibada.
Kwa yeyote ataejaaliwa na kuwa Tayari kujitolea sadaqatul jaaria basi asisite kutoa na Jazaa yako utaikuta mbele ya Haq na Mungu atakupa kheri na thawabu zako. 

Pia unaweza kuwatolea wazazi au ndugu yoyote alie marehem km ni sadaqa kwake na itamfaa sana huko alipo. Kwa mlio Usa au nje ya Tanzania mnaweza kuwasiliana nami Buhite no 12407066333 na mliopo Tanzania number ya Imam na info zaidi zimetajwa hapo juu ktk Clip. Updates zote za hili zoezi tutapost humu na watoaji wote wataorodheshwa pia. Kias kinachohitajika ni Tsh. Million 5 na mpaka sasa imeshakusanywa Tsh. Million 1.5 Tunaomba hata kama ni Dollar 1 usisite kutoa kwani waeza ona ni ndogo kwako lakin hujui kuwa ni kubwa sana kwa mhitaji na jazaa yako utaikuta kwa Allaah Subhanahu Wataala.
Tunapokea mchango toka kwa mtu yoyote hata kama wewe si muislamu lakin ungependa kuchangia ktk kheri hii Tafadhali karibu sana sana.
Natanguliza Shukurani zangu za Dhati kwa wachangiaji na hata wasiojaaliwa kutoa. Mbarikiwe wote.

1 comment:

Anonymous said...

Namba zikowapi? Ukiandikishana bora uweke no kuliko kusubiri mtu atafute clip.Inshaallah Mola atatia Nuru