ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, January 22, 2017

MBOWE KITANZINI TENA, APEWA SIKU 14 KULIPA DENI LINALOMKABILI

Miezi takribani mitano iliyopita tangu aondolewe Billcanas, siku moja tangu Serikali imzuie asiendelee na shughuli za kilimo katika shamba lake, Mwenyekiti huyo wa Chadema amepewa siku 14 awe amelipa kodi inayokadiriwa kufika milioni 13.5, ya hoteli yake ya Aishi iliyoko Machame Mkoani Kilimanjaro.

Uamuzi huo mpya wa Serikali wa Wilaya ya Hai, Mkoani Kilimanjaro,umefikia hatua hiyo ikiwa ni siku moja baada ya Mkuu wa Wilaya hiyo Gellasius Byakanwa, kutangaza kusitisha shughuli za kilimo katika shamba la Veggies analomiliki Mbowe kutokana na kile kilichosema lipo ndani ya chanzo cha maji.

Byakanwa amesema kuwa Serikali ya awamu ya Tano imelenga kukusanya mapato ili iweze kutekeleza majukumu yake ikiwamo kutekeleza ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM).


“Hatuwezi kufikia malengo ya ukusanyaji mapato yetu ya ndani kama kuna wafanyabiashara wakubwa kama huyo wanakwepa kulipa kodi, na tena kwa kipindi chote hicho ameshindwa kuleta hali ya mauzo yake ambayo yataweza kujulikana kiasi anachostahili kulipa kodi,”amesema Byakanwa.

Hata hivyo Mkuu huyo wa Wilaya amemshutumu Mbowe kwa kufanya uharibifu wa mazingira kwa kuvuna miti ya asili bila kibali cha mkuu wa Wilaya kulingana na uamuzi wa Kamati ya ushauri ya Mkoa (RCC) pamoja na kuvuta maji kwa kutumia mashine kinyume na kibali na taratibu za utumiaji wa maji mfereji.

CHANZO: MTANZANIA

No comments: