Advertisements

Monday, January 23, 2017

MBUNGE WA TANGA AWATAKA MADEREVA WA BODABODA KUACHA KUENDESHA MWENDOKASI

MBUNGE wa Jimbo la Tanga (CUF) Mussa Mbaruku (pichani )amewataka  madereva wa pikipiki maarufu kama bodaboda jijini Tanga kuacha kuendesha mwendokasi kwani maisha ya watu yanapotea kwa sababu yao.

Sambamba na hilo amewataka kuondokana na tabia ya kupakia abiria zaidi ya mmoja wanapokuwa barabarani maarufu kama mshikaki kwani jambo hilo ni hatari kwa mustakabali wa maisha yao wanapokuwa njiani.

Mbunge huyo alitoa wito huo  wakati akizungumza na madereva wa pikipiki Kata ya Kirare Jijini Tanga ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya kuwatembelea wananchi na kuangalia changamoto zinazowakabilia kasha kuona namna ya kuzipatia ufumbuzi.

Aliwataka pia kutii sheria za usalama kwa kuvaa kofia ngumu na kuacha kuwa na mbwembwe wanapokuwa barabarani jambo ambalo linaweza kusababisha ajali zinazoweza kugharimu maisha ya watu.

“Lakini pia madereva wa bodaboda hakisheni mnakuwa nadhifu kwa wateja wenu pendeni kazi ikiwemo kuacha kuvaa malapa badala yake wavae viatu vya ngazi “Alisema mbunge huyo.

Hatua ya mbunge hiyo inatokana na kuwepo kwa malalamiko kwa baadhi ya waendesha bodaboda hao kuwa wamekuwa wakikamatwa na askari wa usalama barabarani wanapokuwa kwenye shughuli zao jambo ambalo linasababisha kushindwa kufikia malengo yao.

Bakari Juma ambaye ni mwendesha bodaboda eneo hilo alisema kuwa wamekuwa wakikumbana na wakati mgumu katika kufanya shughuli hizo kutokana na kukamatwa mara kwa mara na kutakiwa kutoa faini.

Naye Zuberi Omari alimuomba mbunge huyo kuangalia namna ya kuwasaidia waendesha bodaboda hao ili waweze kujikwamua kiuchumi kwa kuanzisha chama cha kukopa na kuweka akiba (Saccos) yao ambayo inaweza kuwa mkombozi.

Alisema hivi sasa baadhi ya watu mbalimbali wamekuwa wakianzishya vikundi mbalimbali vikiwemo vya kukopa na kuweka fedha hivyo nasi tungeweza kupata fursa hiyo ingeweza kutusaidia kukabiliana na ugumu wa maisha.

Akizungumzia suala hilo, Mbunge Mussa alisema lazima wahakikisha wanaheshimu sheria za usalama barabara kwa kuacha kuendesha mwendokasi ikiwemo kuwa na leseni za kufanya shughuli hizo ili kuweza kuzifanya kwa usalama zaidi bila kuwepo kwa usumbufu.

Mussa aliwataka pia kuacha kutumia mtindi wa kupakia abiria zaidi ya uwezo wanaakiwa kuwapakia wanaopokuwa kwenye shughuli hizo maarufa kama mshikaki kwani madhara yake ni makubwa sana kwa usalama wao na abiria hao kwani wanaweza kukumbana na ajali ikiwemo kugharimu maisha yao.

 “Leo hii ukiangalia wapo watu ambao wanaendesha vyombo vya moto kama vile bodaboda hawavai elementi lakini wanapakia abiria mishikaki sasa hawa wanakuwa na hatari kubwa kwa usalama barabarani hivyo niwatake muache suala hilo “Alisema.
Habari kwa hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha

No comments: