Advertisements

Tuesday, January 24, 2017

NAIBU WAZIRI MASAUNI AZINDUA UJENZI WA OFISI ZA POLISI KATIKA KIJIJI CHA UTENGULE WILAYANI MBEYA

 Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wapili kulia), akisalimiana na wananchi wa Kijiji cha Utengule, alipowasili kuzindua ujenzi wa jengo litakalotumika kwa ajili ya ofisi za Jeshi la Polisi huku eneo hilo likitolewa na wananchi wa kijiji hicho.Kulia ni Kaimu Kamanda wa Polisi  Mkoa wa Mbeya Emmanuel Lukula.(Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
 Mhandisi wa Wilaya ya Mbeya, Jesse Shengena (kushoto), akimuelekeza Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(katikati) ramani ya Ujenzi wa Jengo litakalotumika  kwa ajili ya ofisi za Jeshi la Polisi katika kijiji cha Utengule wilayani Mbeya. Kulia ni Kaimu Kamanda wa Polisi  Mkoa wa Mbeya Emmanuel Lukula. 
 Kaimu Kamanda wa Polisi  Mkoa wa Mbeya Emmanuel Lukula, akitoa maelezo juu ya Ujenzi wa Jengo litakalotumika kwa ajili ya ofisi za Jeshi la Polisi kwa Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati), eneo la ujenzi wa ofisi hizo limetolewa na wananchi ili kuweza kuimarisha ulinzi katika kijiji hicho cha Utengule wilayani Mbeya.
 Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizindua Ujenzi wa Jengo litakalotumika  kwa ajili ya ofisi za Jeshi la Polisi katika kijiji cha Utengule.Wanaoshuhudia  ni baadhi ya mafundi wakiongozwa na Mhandisi wa Wilaya ya Mbeya, Jesse Shengena (kulia), eneo la ujenzi wa ofisi hizo limetolewa na wananchi ili kuweza kuimarisha ulinzi katika kijiji  cha Utengule wilayani Mbeya.
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza na wananchi wa kijiji cha Utengule  baada ya kuzindua  Ujenzi wa Jengo litakalotumika  kwa ajili ya ofisi za Jeshi la Polisi katika kijiji cha Utengule wilayani Mbeya.Naibu Waziri aliwashukuru wananchi hao kwa kujitolea eneo la kujengwa ofisi za watumishi na askari wa jeshi ikiwa ni juhudi zao katika kupambana na matukio ya uhalifu katika kijiji chao.


IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI-WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

No comments: