Advertisements

Wednesday, January 18, 2017

Obama atoa msamaha wa mwisho kwa wanajeshi

Rais Barrack Obama wa Marekani
Rais Obama amebatilisha kifungo cha jela kwa Chelsea Manning, aliyekuwa mwanjeshi wa Marekani aliyehukumiwa kifungo cha miaka 35 jela kwa kosa la kufichua nyaraka za siri.

Taarifa kutoka ikulu zinasema Manning ataachiwa huru ifikapo mwezi wa tano.

Mwanajeshi huyo aliyekuwa mwanamageuzi alifanya kazi huko Iraq na alikuwa akijulikana pia kama Bradley Manning.

Alipatikana na hatia hiyo mwaka 2013 kwa kuweka karibia robo tatu ya mamilioni ya nyaraka za siri za kijeshi na kidiplomasia katika tovuti ya WikiLeaks.

Rais Obama pia ametoa msamaha kwa mstaafu jenerali James Cartwright, aliyekubali kosa la kutoa taarifa za uongo katika uchunguzi uliokuwa ukifanywa na FBI katika udukuzi wa kompyuta kuhusu mipango ya kinyuklia ya Iran.

No comments: