Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein akisalimiana na Mshauri wa Rais masuala ya Utamaduni Mhe, Chimbeni Kheir Chimbeni jana alipowasili katika viwanja vya Ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi alipohudhuria katika Taarab rasmi ya kusherehekea Miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kushoto) Waziri wa Habari, Utalii, Utamaduni na Michezo Mhe, Rashid Ali Juma (kushoto) Makamo wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Iddi(kulia) na Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe. Kasim Majaliwa Majaliwa (wa pili kulia) pamoja na Viongozi wengine wakiwa katika Ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi katika Taarab rasmi ya kusherehekea Miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar iliyofanyika jana.
Wake wa Viongozi wakuu wa Nchi wakiwa katika Ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi katika Taarab rasmi ya kusherehekea Miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar iliyofanyika jana iliyopigwa na Kikundi cha Taifa.
Baadhi ya Viongozi na Waalikwa mbali mbali wakiwa katika Ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi katika Taarab rasmi ya kusherehekea Miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar iliyofanyika jana iliyopigwa na Kikundi cha Taifa.
Kikundi cha Taifa cha Muziki wa Taarab kikitumbuiza kwa Wimbo unaosema "Khofu yako Iondoke"ilyoimbwa na Profesa Moahmed Ilyas katika sherehe za Taarab rasmi ya kusherehekea Miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar iliyofanyika jana, mgeni rasmi akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein (Picha na Ikulu).
No comments:
Post a Comment