Advertisements

Friday, January 13, 2017

SERIKALI YAUNDA TUME KUBAINI CHANZO CHA MOTO JNIA

 Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akikagua sehemu ya kuhifadhia mizigo ya abiria kilivyoteketea kwa moto  usiku wa kuamkia leo katika Kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Mwalimu Julius Nyerere ,kulia ni Mkurugenzi wa Uwanja huo Bw. Paul Rwegasha.
 Mkurugenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Mwalimu Julius Nyerere Bw. Paul Rwegasha akimuonesha Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa chumba cha kuhifadhia mizigo ya abiria kilivyoteketea kwa moto usiku wa kuamkia leo.
 Mkurugenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Mwalimu Julius Nyerere Bw. Paul Rwegasha akimuonesha Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa chumba cha kuhifadhia mizigo ya abiria kilivyoteketea kwa moto usiku wa kuamkia leo.
 Mkurugenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Mwalimu Julius Nyerere Bw. Paul Rwegasha akimuonesha Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa chumba cha kuhifadhia mizigo ya abiria kilivyoteketea kwa moto usiku wa kuamkia leo.
Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akisisitiza jambo kwa wanahabari (hawapo pichani) mara baada ya kukagua chumba cha kuhifadhia abiria kilichoteketea kwa moto usiku wa kuamkia leo (jana),wa kwanza kulia ni Kaimu Katibu Mkuu Sekta ya Uchukuzi Bw. Gabriel Migire. (Picha na Benjamin Sawe-Maelezo).

Serikali imesema imeunda Tume ya uchunguzi ya watu 12 ili kuweza kuchunguza na kubaini chanzo cha ajali ya moto iliyotokea jana saa Tano usiku katika chumba kidogo cha kuhifadhia mizigo kilichopo kwenye jengo la Pili la abiria (Terminal II) katika uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam leo, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa amesema kuwa  Tume hiyo iliyoundwa inaongozwa  na Joseph Nyahende ambae anatoka katika ofisi za  Makao Makuu ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege nchini.
“Ninategemea kupata ripoti ya kitaalamu kutoka kwa Tume hii, ili kutusaidia kubaini kiundani juu ya chanzo haswa kilichopelekea moto huu”, amesema Waziri Mbarawa.
Aidha, Waziri Mbarawa amefafanua kuwa huduma katika jengo hilo  zinaendelea kama kawaida ambapo awali zilisitishwa na kuhamishiwa katika Jengo la Kwanza la abiria (Terminal I).
“Mara baada ya moto kutokea, kitu cha kwanza kilichofanyika ni kuudhibiti moto huu ili usiweze kusambaa katika maeneo ambayo hayajaathirika, kisha tukatafuta njia za kurudisha huduma kwa abairia”, amesisitiza Profesa Mbarawa.
Katika hatua nyingine, Profesa Mbarawa ameipa miezi miwili  kampuni ya mizigo ya Swissport kurekebisha huduma zinazolalamikiwa na wateja wake na endapo itashindwa hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Uwanja wa Ndege wa JNIA, Paul Rwegasha ameeleza kuwa tathmini na gharama za mizigo iliyokuwa imehifadhiwa katika chumba hicho bado haijajukana, ambapo ripoti itaeleza gharama hizo pindi itakapokamilisha uchunguzi wake.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

1 comment:

Anonymous said...

Kwani hatuna forensic experts katika jeshi letu la polisi? Hizi tume kuanzia zinapoundwa mpaka matokeo yapatikane gharama zake zitazidi hasara iliyopatikana. At the end utaambiwa kuwa "ilikuwa ni hitilafu ya umeme".