Advertisements

Wednesday, January 11, 2017

WAKILI ATAKA MKE WA BILIONEA MSUYA AACHIWE HURU

Wakili John Malya ameiomba Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu iwaachie huru washtakiwa, Miriam Stephen Mrita (41)na Revocatus Evarist Muyela (40) wanaokabiliwa na kesi ya mauaji ya dada wa marehemu bilionea Erasto Msuya, Aneth Msuya kwa sababu kwa hakuna hati ya mashtaka inayowashikilia washtakiwa hao mahakama hapo.
Malya alilitoa ombi hilo leo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Godfrey Mwambapa baada ya Wakili wa Serikali Mwandamizi, Kishenyi Mutalemwa kuiomba mahakama iwape muda ili waweze kutekeleza amri ya mahakama iliyotolewa Januari 9, 2017.
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu iliamuru washtakiwa hao wa kesi hiyo ya mauaji ya Aneth Msuya wapewe PF3 ndani ya siku mbili, wakatibiwe baada ya kukubaliana na madai yao kuwa walipigwa wakati wakiwa mahabusu katika kituo cha Polisi na kwamba hati ya mashtaka inayowakabili mahakamani hapo ni mbovu hivyo ifanyiwe marekebisho.
Baada ya Wakili Kishenyi kuomba muda wa kutekeleza amri hizo za mahakama, Wakili Malya aliiambia mahakama kuwa amri ya mahakama ni sheria na upande wa mashtaka umekataa kutekeleza sheria hiyo,washtakiwa wanashikiliwa bila ya kuwa na hati yoyote inayowashikilia mahakamani hapo hivyo aliomba waachiwe huru.

No comments: