ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, January 19, 2017

WAKUU WA MASHIRIKA YA UMEME KUTOKA NCHI KUMI ZA EASTERN AFRICA WAKUTANA ARUSHA KUJADILI NAMNA YA KUUNDA MIFUMO YA USAFIRISHAJI UMEME KWA NCHI HIZO


Na Woinde Shizza,Arusha

Wakuu wa  mashirika umeme kutoka katika nchi kumi za Afrika zinazozalisha
umeme(Eastern Africa Power pool(EAPP)          zimekutana  jijini arusha
kwa malengo ya kujadili mfumo wa usafirishaji wa umeme ikiwa ni pamoja na
namna wananchi wao watakavyoweza pata nishati ya umeme kwa uraisi tofauti
na sasa

Hayo yalisemwa na naibu katibu mkuu wizara ya nishati na madini Dkt.Juliana
palangyo alipokuwa akizungumza katika ufunguzi wa mkutano wa wakuu wa
mashirika ya umeme katika nchi hizo za eastern Africa power
pool(eapp)mapema leo

Palangyo alisema kuwa lengo halisi ni kuweza kujadili mambo mbalimbali
yahusuyo nishati ya umeme kwa watumiaji wake kwani  kuna uwezekano  mkubwa
wa nchi zote zilizo kwenye umoja huo.

Alisema kwa sasa yapo baadhi ya makampuni ambayo yalikuwa yanauza umeme kwa
gharama kubwa hasa kwa wananchi ambao hawajapata huduma hiyo ya umeme


lakini kupitia umoja huo wataweza kupata nishati hiyo kwa gharama nafuu.

"Hizi nchi za eastern tumekutana hapa ili tujadili namna ambayo tunaayo
wanayoweza kutafuta namna ya kuzalisha umeme kwa bei nafuu na kisha nchi
hiyo itaweza kuuza umeme  kwa bei ndogo"aliongeza palangyo.

Hataivyo kwa upande  kaimu meneja uhusiano wa shirika la tanesco  Leila
Muhaji alisema kuwa katika mkutano huo pia watajadili namna ambavyo
tanzania itajenga njia ya usafirishaji wa umeme wa njia ya maji ambayo
itatoka nchi ya tanzania kwends kenya,zambia,pamoja na nchi nyingine

Muhaji alisema kuwa tanzania itanufaika na ujenzi wa njia hizo hivyo jamiii
itanufaika kwa kiwango kikubwa sana kama ilivyo kwenye nchi ambazo
zimeeendelea duniani.

"Hataivyo mara baada ya huu mkutano wa wakuu wa nchi zinazolisha umeme
tunatarajia pia kuwepo na wadau wengine ambao ni mawaziri kutoka nchi zote
ambao nao sasa wataweza kuweka mambo sawa ili huduma iweze kumfikia
mlengwa"aliongeza Muhaji

Alimalizia kwa kutaja nchi ambazo zina unda umoja huo kuwa ni  Tanzania ,Kenya,Uganda ,Rwanda ,Burundi ,Sudan , Dr congo, Ethiopia ,Djbout, Libya pamoja na Egypt.

No comments: