ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, January 19, 2017

WAZIRI NAPE ATEMBELEA IDARA YA HABARI (MAELEZO NA KUZUNGUMZA NA WAFANYAKAZI

 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Mozes Nnauye akipokelewa na Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZ0) Dkt. Hassan Abbasi (kushoto) alipofanya ziara katika ofisi za Idara hiyo leo jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Dkt. Hassan Abbasi akielezea jambo kwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (wa kwanza kulia) leo jijini Dar es Salaam. Waziri Nape amefanya ziara katika Ofisi za Idara ya Habari (MAELEZO) kwa lengo la kusikiliza changamoto za wafanyakazi wa idara hiyo.
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Mozes Nnauye akifafanua jambo alipotembelea Ofisi za Idara ya Habari (MAELEZO) leo jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZ0) Dkt. Hassan Abbasi, Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa Wizara hiyo Bibi. Zawadi Msala na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari (Sehemu ya Habari) Bw. Artemony Tiganya.
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Mozes Nnauye akiangalia makabati yanayohifadhia majarada ya usajili wa magazeti alipotembelea Ofisi za Idara ya Habari (MAELEZO) leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari (Sehemu ya Habari) Bw. Artemony Tiganya.
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Mozes Nnauye akiangalia saver kwa ajili ya kuhifadhi Picha za matukio mbalimbali alipotembelea Ofisi za Idara ya Habari (MAELEZO) leo jijini Dar es Salaam. kulia ni Afisa Habari Mkuu wa Idara hiyo Bw. John Lukuwi.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Mozes Nnauye akiangalia akiangalia mfumo wa zamani wa kuhifadhia magazeti alipotembelea Ofisi za Idara ya Habari (MAELEZO) leo jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa Wizara hiyo Bibi. Zawadi Msalla  na Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Dkt. Hassan Abbasi, Katibu wa Waziri Bw. Octavian na Afisa Habari Mkuu John Lukuwi.
 Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Dkt. Hassan Abbasi akimuonyesha habari iliyoandikwa katika gazeti la Mzalendo la miaka ya nyuma Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (kulia) alipotemmbelea Ofisi za Idara hiyo leo jijini Dar es Salaam.
 Afisa Habari Mkuu wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bw. John Lukuwi akimuelezea Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Mozes Nnauye ( aliyekaa) namna Kamera ya kupigia picha za majengo marefu inavyofanya kazi wakati wa ziara yake katika Ofisi za Idara hiyo leo jijini Dar es Salaam. Waliosimama wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Dkt. Hassan Abbasi na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara hiyo (Sehemu ya Habari) Bw. Artemony Tiganya.
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye(watatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa Idara ya Habari (MAELEZO) mara baada ya kumaliza kikao leo jijini Dar es Salaam.
Picha zote na: Frank Shija – MAELEZO.

No comments: