Na Mwandishi wetu, Washington, DC
Wamarekani wakiandamana katika moja ya viwanja vya ndege vya kimataifa kupinga mswada mpya wa uhamiaji uliotiwa saini siku ya Ijumaa Januari 27, 2017 kuzuia kuingia nchini Marekani kwa raia kutoka nchi za Syria, Iraq, Iran, Somalia, Sudan, Yemen na Libya.
Katika mswada huo uliwajumlisha hata raia wa nchi hizo waliokua na ukaazi wa kudumu yaani Green Cards, wanataikiwa wasingie nchini wakiwemo waliopata VISA za aina yeyote. Zuio hilo ni kwa siku tisini kwa lengo la usalama wa Marekani.
Tangia mswada huo usainiwe siku ya Ijumaa na kuanza kutumika mara tu baada ya kusainiwa kwake, mashirika ya ndege yalikataa kuwachukua raia wa nchi hizo na wale waliokua ndani ya ndege tayari kuzuiliwa kuingia nchini Marekani.
Mswada huo pia uliwahusisha wakimbizi wanaotoka nchi hizo kusitishwa kuingia Marekani kitu ambacho kilipingwa vikali na watu kuandamana kwenye viwanja vya ndege vya kimataifa karibu majimbo yote na kusababisha baadhi ya viwanja kufungwa kwa muda kwa wingi wa waandamanaji hao.
Msemaji wa Homeland Security amefafanua kuhusu wananchi wenye makazi ya kudumu kwamba mswada huo umetafusiliwa vibaya, mswada huo haumzuii raia mwenye green card kuingia nchini lakini kuhusu wakimbizi na wale wote wenye VISA za kuingia nchini Marekani ndio wamezuiliwa kwa muda wa miezi 3 mpaka hapo itakapotangazwa tena na si kwa ajili ya Uislamu ni kwa ajili ya usalama wa Marekani.
Hali ikiwa tete kwenye viwanja vya ndege vya kimataifa waandamaji wakiandamana kuppinga mswada mpya uliosainiwa na Rais Donald Trump siku ya Ijumaa kuzuia raia wa nchi 7 za Kiislam kuingia nchi Marekani wakiwemo wakimbizi wa nchi hizo kwa siku 90.
Waandamanaji wakiwa moja ya kiwanja cha ndege cha kimataifa.
Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Los Angeles.
No comments:
Post a Comment