Wanawake nchini Marekani siku ya Jumaosi Jan 21, 2017 walifanya maandamano ya amani majimbo yote ya Marekani huku wakiongzwa na wasanii wakubwa wa muziki na sinema kumpinga Rais Trump ambaye aliapishwa siku ya Ijumaa jan 20, 2017 kuwa Rais wa 45 wa marekani. Ushindi wa Rais Trump umekua gumzo kila kona ya Dunia huku wengi wakipigwa na butwaa kwa ushindi ambao hakuna mtu aliyeutarajia na FBI wakiwa wanaendelea na uchunguzi kutaka kufahamu kama komputa za uchaguzi ziliingiliwa kwa ajili ya kupanga matokeo ya kura za Electoral College ambazo ndizo zinazompa ushindi Rais wa Marekani hata kama umeshindwa idadi ya kura zilizopigwa na wananchi.
Uchaguzi uliopita Hillary Clinton ameshinda zaidi ya kura milioni 3 ya jumla ya kura zote zilizopigwa na wananchi wa Marekani lakini kutokana na Rais Donald Trump kushinda kwenye kura za Electoral College ambazo ndizo zinazomchagua Rais wa Marekani.
Wanawake wakiandamana nchini Marekani kupinga RaisTrump kuingia madarakani.
w
Idadi kubwa ya wanawake walioandamana katika majimbo ya Marekani kumpinga Rais Trump ambaye sasa anailaumu media kwa kumpiga vita.
Wanawake jimbo la Florida wakiandamana na mabango yao.
No comments:
Post a Comment