MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya
Mkoa Tanga (NHIF) umefanikiwa kutoa
mikopo ya vifaa tiba na ukarabati katika vituo vya afya na
hospitali vyenye thamani ya
Milioni 559.2.
Vituo ambavyo vilikopeshwa ni Hospitali ya Mkoa wa Tanga Bombo, Hospitali za wilaya ya Korogwe,
Lushoto, Handeni ikiwemo vituo vya
Afya Makorora, Kituo cha Afya Pongwe, Mikanjuni na Ngamiani.
Hayo yalisemwa hivi karibuni na Meneja wa Mfuko huo mkoani hapa,
Ally Mwakababu (Pichani Juu)wakati akielezea
taarifa ya utendaji kwa waandishi wa habari mjini hapa
Alisema baadhi ya vituo vya afya vilivyokopeshwa na mfuko huo
kati yao vinne vimemaliza
kurejesha mikopo yao ambavyo ni Hospitali ya wilaya ya Pangani,Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga
Bombo (mkopo wa awali) na
kituo cha Afya cha Besha na Makorora ambapo ni mkopo wa
awali.
Meneja huyo alisema licha ya kuwepo kwa uhamasishaji mkubwa
wanaoufanya lakini vituo vingi havijachangamkia fursa hiyo ya
mikopo ya vifaa tiba,
ukarabati wa majengo na dawa.
“Hivyo nivisihi vituo kujitokeza kuchangamkia fursa hii ya mikopo
ya vifaa tiba, ukarabati wa
majengo na dawa kwenye maeneo yao “Alisema Meneja huyo.
Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha.
No comments:
Post a Comment