Bunge limepitisha maoni na mapendekezo ya kamati ya kudumu ya bunge ya bajeti yanayotaka serikali kufanya zoezi la tathimini ya kina juu ya uwezo wa nchi wa kukopa na kulipa madeni bila ya kuathiri fedha za miradi ya maendeleo nchini.
Akiwasilisha maoni,changamoto na mapendekezo ya kamati hiyo, Makamu Mwenyekiti wa kamati Bunge ya bajeti Mhe Josephat Kandege amesema kamati hiyo imetaka serikali kuhakikisha ukopaji wa mikopo ya ndani usizidi kiwango kilicho idhinishwa na bunge na uzingatie hali ya uchumi na ukwasi wa mabenki katika kipindi husika.
Akijibu hoja wa wabunge wa kutaka kuongeza fedha zaidi katika sekta ya kilimo,Waziri wa fedha na mipango, Mhe Dkt Phillip Mpango amesema kuongezwa bajeti pekee ya kilimo kutabadilisha kilimo nchini haiwezekani kutokana na sekta ya kilimo kutegemea sekta nyingine zaidi ili kiweze kufanya vizuri.
Wakichangia katika mkutano huo baadhi ya wabunge wametaka serikali kuangalia upya sera za kodi na kuzifanya kuwa rafiki kwa mlipa kodi ili kuondoa tatizo la walipa kodi kujitahidi kukwepa kutokana na ukubwa wa kodi hizo kuliko gharama ununuzi wa bidhaa.
No comments:
Post a Comment