katika historia ya mkoa kagera itambulike na ijulikane kuwa ndio mkoa pekee wenye kupatwa na majanga tena yenye kuumiza na kuuzunisha kwa kila utawala wa kiingozi Mkuu wa nchi.
1978/1979
historia inaonesha kwamba mkoa huo ulikumbwa na vita,ndugu ,jamaa na wanafamilia wetu wakapoteza maisha lakini haikuwa tuu kuutetea mkoa huo bali ilikuwa ni kurudisha heshima ya nchi yetu
"Utawala wa hayati *Mwl JK.NYERERE"
1980/1985
historia ikaonesha kuwa mkoa huo uligubikwa na janga sugu la *UKIMWI.* Vilio, majonzi na misiba ikawa kila familia. maeneo yaliyoathirika sana yalikuwa ni *KANYIGO,KAMACHUMU na MULEBA.
"Utawala wa ALL HASAN MWINYI"
1996
historia inaonesha kwamba ndugu zetu zaidi *10000* walipoteza maisha katika tukio la kuzama kwa *MV BUKOBA (TIKILIWA IGAMBA)* hakika yatupasa kujiuliza ,kwanini *BUKOBA??
1997
historia ikaandika kuwa zaidi ya watu kupoteza maisha katika kipindi cha *ELMINO* mafuriko yakawa shida.
"Utawala wa *BENJAMIN WILLIUM MKAPA"
2001-2003
palitokea kiangazi au ukame uliozidi kiwango mifugo,mashamba na mazao ikiwa ni MAJINAMIZI. *Wanakaragwe ,muleba,kyerwa,ngara* ,nina imani kuwa mnayo hiyo kumbukumbu nyama ya ng'ombe ikauzwa kwa *Tsh.1500/=*
2012-2014
kimbunga kiliutawala mkoa huo ikaandikwa kuwa historia tena,majumba yaliezuliwa,migomba ukaanguka,watu wakakoswa malazi,chakula hata miundo mbinu. Tibaijuka ANNA akatoa msaada wa vyakula,blanketi,mabati,hata madawa MAMA TUNAKUSHUKURU KWA HILO.
"Utawala wa JK "
2015
MWEZI WA SABA takribani watu 600 walinusurika kifo baada ya *MV SERENGETI* kushindwa kutia nanga katika kasitamu ya *KEMONDO* ilipepesuka kwa muda ulidumu masaa 6 tunawashuru sana MASHEKHE,MAPADRE,WACHUNGAJI na wale wote walitoa muda wako kuomba kwa MUNGU ili aepushe janga hilo.
10/09/2016
historia ikaandikwa tena katika mkoa huohuo *TETEMEKO LA ARDHI* lililozua taharuki na sintofahamu katika Akili, imani na fikra za wakazi wa mkoa kagera kwa kushuhudia madhara makubwa yalitokea majumba kuporomoka,milima na vilima vikijihamisha kutoka sehemu kwenda sehemu , hofu ikatanda juu hatima ya maisha ya ndugu zetu.
Hakika vifo vimetokea ,miundo mbinu kuharibiwa hata mifugo kufa.
Leo imebidi nijifunze lugha yao ili kuwapa pole.
"NYARUJU WAITU NYARUJU, KATONDA EYATONZILE NAIGULU. NITUKUSHABA EBIKOLWA BYAWE OTUGANYILE"
No comments:
Post a Comment