ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, February 7, 2017

JENERALI MWAMNYANGE ATAJA KITU AMBACHO HATOKISAHAU

Aliyekuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Davis Mwamunyange, amesema katika kipindi chake cha utumishi jeshini, hatasahau kamwe tukio la milipuko ya mabomu kwenye vikosi vya Mbagala mwaka 2009 na Gongolamboto mwaka 2011.

Aliyazungumza hayo Ikulu, Dar es Salaam Jumatatu hii wakati akiongea na wanahabari baada ya kuapishwa mkuu mpya wa majeshi, Jenerali Venance Mabeyo. Jenerali mstaafu Mwamunyange alisema tangu aingie jeshini mwaka 1971, wakati wa milipuko hiyo iliyosababisha vifo na uharibufu wa mali, ndiyo ulikuwa mgumu zaidi kwake.
“Wakati wa milipuko ya Mbagala na Gongolamboto nilikuwa kwenye nafasi hii (Mkuu wa Majeshi), huu ndiyo ulikuwa wakati mgumu kwangu kwa sababu ilisababisha vifo, mali za watu na askari ziliteketea, kwangu kipindi kile kilikuwa kigumu sana,” alisema Mwamunyange.
Milipuko ya mabomu ya Mbagala, ilitokea April 2009, kwa upande wa Gongo la Mboto ilitokea Februari 2011.

No comments: