Advertisements

Tuesday, February 21, 2017

KAMISHNA JENERALI WA JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI TANZANIA BARA ATEMBELEWA NA KAMISHNA JENERALI WA JESHI LA UHAMIAJI

Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye atembelewa na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Uhamiaji Dkt. Anna Makakala lengo ni kujifunza na kukuza mahusiano kati ya vyombo hivyo viwili vya Ulinzi na Usalama.

Katika ziara hiyo Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye, alitumia fursa hiyo kumpongeza kwa kuteuliwa na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kuwa Kamishna Jenerali wa Jeshi la Uhamiaji na kumuahidi ushirikiano katika kulijenga Taifa. Kamishna Jenerali wa Jeshi la Uhamiaji Dkt. Anna Makakala ametembelea Makao Makuu ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji yaliyopo jengo la ushirika - mnazi mmoja jijini Dar es salaam, mapema leo asubuhi na alipata fursa ya kujifunza jinsi gani Jeshi hilo linavyoendesha shughuli zake pamoja na kuwa na mazungumzo ya kina na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji pamoja na Viongozi Waandamizi wa Jeshi hilo. “Nimejifunza mengi lakini pia nashukuru kwa kupata fursa ya kutembelea na kuona ni jinsi gani tunaweza kushirikiana” alisema Kamishna Jenerali wa Jeshi la Uhamiaji Dkt Anna Makakala.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Uhamiaji Dkt. Anna Makakala (kulia) akisaini kitabu cha wageni alipotembelea Makao Makuu ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mapema leo asubuhi (kushoto) ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye aliyekaa katikati mbele akiwatambulisha Viongozi Waandamizi wa Jeshi hilo kwa Kamishna Jenerali wa Jeshi la Uhamiaji Dkt. Anna Makakala na kumueleza ni jinsi gani Jeshi la Zimamoto linavyoendesha shughuli zake.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye akimkabidhi zawadi ya bendera ndogo ya mezani Kamishna Jenerali wa Jeshi la Uhamiaji Dkt. Anna Makakala ikiwa ni ishara ya umoja, ushirikiano na ukumbusho juu ya ziara yake alipotembelea Makao Makuu ya Jeshi hilo jengo la ushirika – mnazi mmoja mapema leo asubuhi.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye (kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Uhamiaji Dkt. Anna Makakala (kulia) mapema leo asubuhi alipotembelea Makao Makuu ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye akiwa kwenye picha ya pamoja na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Uhamiaji Dkt. Anna Makakala na Viongozi Waandamizi wa Jeshi la Zimamoto mapema leo asubuhi.

(PICHA NA FC GODFREY PETER)

No comments: