ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, February 21, 2017

PRESS RELEASE: HUSSEIN MACHOZI KUVUNJA UKIMYA NA ‘NIPE SIKUACHI’ CHINI YA COMBINATION SOUND

Dar es Salaam, Tanzania, February 21, 2017

Baada ya kukaa kimya kwa miezi mingi bila kuachia wimbo, Hussein Machozi anatarajia kuachia wimbo mpya wiki chache zijazo. Wimbo huo unajulikana kwa jina la ‘Nipe Sikuachi.’

Wimbo huo umetayarishwa na mshindi wa tuzo ya mtayarishaji bora wa Bongo Flava katika miaka tofauti, Man Walter kupitia studio zake za Combination Sound.

“Combination yangu ya mimi na Man Walter, sidhani kama kuna kitu cha mchezo hapo,” anasema Machozi ambaye amethibitisha kuanza kufanya kazi rasmi kwa uangalizi wa label ya mtayarishaji huyo mashuhuri nchini Tanzania.

“Man Walter ni mshkaji kitambo, tumekutana tukakubaliana kufanya kazi na tukaona kabisa kwamba sisi tukifanya kazi wawili itakuwa kazi na ndicho kilichofanyika japo tuna makubaliano ya kusaini. Kwahiyo ni mimi tu nirudi Tanzania tuje tukae tusaini, lakini ukweli ni kwamba mimi nafanya kazi chini ya uongozi wa Kombinega,” amesema.

“Video pia imefanyika Italy, Gressoney Italy. Kuna mabadiliko makubwa ukiangalia location ambazo tumezizoea, ukiangalia video ambazo kila siku tunaziona Tanzania za magari na majumba,” amesisitiza muimbaji huyo.

Machozi ambaye anafahamika kwa vibao vingi vilivyowahi kufanya vizuri kwenye vituo vya redio na runinga ndani na nje ya Tanzania vikiwemo ‘Utaipenda’, ‘Kwaajili Yako’, ‘Addicted’ na zingine, amedai kuwa ukimya wake ulitokana na majukumu mengine ya kimaisha.

“Kama unavyojua, hakuna mtu anapenda kuwa kimya, na ukifuatilia vizuri kuna kazi kadhaa nilishawahi kuziachia lakini hazikufika nilikotarajia nadhani kwasababu ya ukosefu wa management.

Kwa sasa Hussein anaishi nchini Italia baada ya kuwa ameenda kusoma, lakini hiyo haimaanishi kuwa ameupa kisogo muziki, kitu anachoamini alizaliwa kukifanya.

“Ilikuwa ni kozi fupi ambayo kwa sasa imeisha na nafanya shughuli za kawaida kujipatia riziki,” anaeleza.

Machozi anakikisha kuwa ujio wake mpya utakuwa wa tofauti.

“Kinachokuja kuonekana sasa hivi, hakijawahi kuonekana katika macho ya watu na nimejaribu kufanya hivyo kwasababu mimi mwenyewe nahitaji mabadiliko, nifanye kitu ambacho ni kipya zaidi hata kwenye macho yangu mimi, kwahiyo nimekikubali kwamba ni kipya, video ni mpya, audio ni mpya kabisa.”

Anasema tarehe rasmi ya kutoka kwa video na wimbo itatangazwa hivi karibuni.

KUFAHAMU ZAIDI KUHUSU HUSSEIN MACHOZI MFUALITIE KWENYE MITANDAO YA KIJAMII:

https://www.instagram.com/husseinmachozi100/
https://www.facebook.com/Hussein-Machozi
https://twitter.com/MachoziHussein

UKITAKA MAHOJIANO NAYE WASILIANA NAMI:

fred@bongo5.com
Fredrick Bundala
Publicist (Hussein Machozi & More)
Next Move PR
0785413163

No comments: