Advertisements

Tuesday, February 21, 2017

KATIBU WA SEKRETARIETI YA KITAIFA YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA BIASHARA HARAMU YA BINADAMU NCHINI AWATAKA WANASHERIA KUONGEZA KASI USIKILIZAJI KESI ZA BIASHARA HIYO HARAMU


Katibu wa Sekretarieti ya Kitaifa ya Kuzuia na Kupambana na Biashara Haramu ya Binadamu kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Separatus Fella, akitoa hotuba ya kufunga Mafunzo yaliyoandaliwa na Taasisi ya Wanasheria Wasio na Mipaka (Lawyers Without Borders) ya nchini Marekani. Mafunzo hayo yaliratibiwa na Wizara hiyo ambapo yalitolewa kwa Maafisa Wapelelezi wa Jeshi la Polisi, Mahakimu na Waendesha Mashtaka (hawapo pichani) kwa kupewa uelewa na mbinu ya Kupeleleza, Kuendesha na Kusikiliza kesi dhidi ya Biashara Haramu ya Usafirishaji Binadamu. Mafunzo hayo ya siku tano yalifanyika katika Ukumbi wa Mikutano, Hoteli ya Land Mark, jijini Dar es Salaam. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.


Katibu wa Sekretarieti ya Kitaifa ya Kuzuia na Kupambana na Biashara Haramu ya Binadamu kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Separatus Fella (kushoto), akipokea kitabu kinachoelezea Biashara Haramu ya Usafirishaji Binadamu, kutoka kwa Jaji wa Mahakama Kuu nchini Marekani, Virginia Kendall. Taasisi ya Wanasheria Wasio na Mipaka (Lawyers Without Borders) ya nchini Marekani, waliandaa mafunzo kwa Maafisa Wapelelezi wa Jeshi la Polisi, Mahakimu na Waendesha Mashtaka kwa lengo la kutoa uelewa na mbinu ya Kupeleleza, Kuendesha na Kusikiliza kesi dhidi ya Biashara Haramu ya Usafirishaji Binadamu. Mafunzo hayo ya siku tano yalifanyika katika Ukumbi wa Mikutano, Hoteli ya Land Mark, jijini Dar es Salaam.

Jaji wa Mahakama Kuu nchini Marekani, Virginia Kendall, akizungumza na Maafisa Wapelelezi wa Jeshi la Polisi, Mahakimu na Waendesha Mashtaka (hawapo pichani) kabla ya kufungwa mafunzo ya kutoa uelewa na mbinu ya Kupeleleza, Kuendesha na Kusikiliza kesi dhidi ya Biashara Haramu ya Usafirishaji Binadamu kwa Maafisa hao. Mafunzo hayo yaliandaliwa na Taasisi ya Wanasheria Wasio na Mipaka (Lawyers Without Borders) ya nchini Marekani na kuratibiwa na Sekretarieti ya Kitaifa ya Kuzuia na Kupambana na Biashara Haramu ya Binadamu, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. Mafunzo hayo ya siku tano yalifanyika katika Ukumbi wa Mikutano, Hoteli ya Land Mark, jijini Dar es Salaam.

Katibu wa Sekretarieti ya Kitaifa ya Kuzuia na Kupambana na Biashara Haramu ya Binadamu kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Separatus Fella, akitoa hotuba ya kufunga Mafunzo yaliyoandaliwa na Taasisi ya Wanasheria Wasio na Mipaka (Lawyers Without Borders) ya nchini Marekani, kwa Maafisa Wapelelezi wa Jeshi la Polisi, Mahakimu na Waendesha Mashtaka kwa kupewa uelewa na mbinu ya Kupeleleza, Kuendesha na Kusikiliza kesi dhidi ya Biashara Haramu ya Usafirishaji Binadamu. Mafunzo hayo ya siku tano yalifanyika katika Ukumbi wa Mikutano, Hoteli ya Land Mark, jijini Dar es Salaam


Jaji wa Mahakama Kuu nchini Marekani, Virginia Kendall akimpa Afisa wa Sekretarieti ya Kitaifa ya Kuzuia na Kupambana na Biashara Haramu ya Binadamu kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Happyness Laizer (kulia), cheti cha ushiriki wa mafunzo ya Maafisa Wapelelezi wa Jeshi la Polisi, Mahakimu na Waendesha Mashtaka kabla ya Mafunzo hayo ambayo yalilenga kutoa uelewa na mbinu ya Kupeleleza, Kuendesha na Kusikiliza kesi dhidi ya Biashara Haramu ya Usafirishaji Binadamu ambayo yaliandaliwa na Taasisi ya Wanasheria Wasio na Mipaka (Lawyers Without Borders) ya nchini Marekani, kufungwa. Mafunzo hayo ya siku tano yalifanyika katika Ukumbi wa Mikutano, Hoteli ya Land Mark, jijini Dar es Salaam.


Katibu wa Sekretarieti ya Kitaifa ya Kuzuia na Kupambana na Biashara Haramu ya Binadamu kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Separatus Fella (kulia), Afisa wa Sekretarieti hiyo, Happyness Laizer (wapili kulia), wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Maafisa wa Taasisi ya Wanasheria Wasio na Mipaka (Lawyers Without Borders) ya nchini Marekani, mara baada ya Mafunzo yaliyoandaliwa na Taasisi hiyo yaliyotolewa kwa Maafisa Wapelelezi wa Jeshi la Polisi, Mahakimu na Waendesha Mashtaka kufungwa. Mafunzo hayo yaliratibiwa na Secretarieti hiyo na kufanyika katika Ukumbi wa Mikutano, Hoteli ya Land Mark, jijini Dar es Salaam.

Na Felix Mwagara, MOHA

KATIBU wa Sekretarieti ya Kitaifa ya Kuzuia na Kupambana na Biashara Haramu ya Binadamu kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Separatus Fella, amewataka Maafisa Wapelelezi wa Jeshi la Polisi, Mahakimu na Waendesha Mashtaka nchini watumie mbinu za kisasa za Kupeleleza, Kuendesha na Kusikiliza kesi dhidi ya Biashara Haramu ya Usafirishaji Binadamu.

Akuzungumza katika Hoteli ya land Mark, iliyopo Mbezi Beach, jijini Dar es Salaam wakati akifunga mafunzo ya siku tano kwa wanasheria hao yaliyoandaliwa na Taasisi ya Wanasheria Wasio na Mipaka (Lawyers Without Borders) ya nchini Marekani, Fella alisema, Tanzania ni kati ya mataifa yanayoshamiri kwa biashara hiyo hivyo mafunzo yaliyotolewa na Taasisi hiyo yataleta mwanga zaidi kwa wanasheria hao nchini.

“Nawaomba washiriki wote wa mafunzo haya, kuzingatia na kutumia kwa usahihi utaalamu mlioupata katika kupambana na tatizo hili la biashara haramu ya usafirishaji wa binadamu ambalo linaendelea kukua kwa kiwango kikubwa,” alisema Fella.

Fella aliongeza kuwa, Tanzania ni kati ya mataifa yanayoshamiri kwa biashara haramu ya ikiwemo ya usafirishaji watoto ikiwa na lengo la kwenda kuwatumikisha kazi katika maeneo mbalimbali nchini pamoja na duniani kwa ujumla, kutokana na changamoto hiyo, Serikali ina mipango mbalimbali ya kupambana na tatizo hilo ambalo linazidi kukua kila siku.

Hata hivyo, Fella alisema licha ya changamoto mbalimbali ya kupambana na biashara hiyo, lakini ofisi yake imejipanga kikamilifu kupambana na biashara hiyo kwani maafisa wake wana ujuzi na wanaendelea kupata ujuzi wa kupambana na biashara hiyo na pia wanaendelea kutumia nyenzo mbalimbali za utoaji elimu kwa umma juu ya matatizo hayo nchini.

Kwa upande wake, Jaji wa Mahakama Kuu nchini Marekani, Virginia Kendall ambaye ni mmoja kati ya wataalamu waliotoa mafunzo kwa maafisa hao, aliishukuru Serikali ya Tanzania kwa kutoa kipaumbele cha upambanaji wa biashara hiyo haramu na pia elimu waliyoitoa wataalamu hao kwa wanasheria hapa nchini itasaidia kuongeza kasi kubwa ya kupambana na biashara hiyo.

Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi iliratibu mafunzo hayo kwa lengo la kujipanga kikamilifu katika kupambana na biashara hiyo haramu ambayo inazidi kuleta mateso makubwa kwa idadi kubwa ya Watanzania.

Pia Mwezi Oktoba mwaka jana, Wizara hiyo iliandaa Warsha ambayo ilifadhiliwa na Umoja wa Ulaya (EU) pamoja na Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) ambayo ililenga kujadili nyenzo mbalimbali ambazo zitasaidia kuwalinda na kuwasaidia watoto walioathirika na biashara ya kusafirisha binadamu nchini.

Nyenzo hizo zililenga kuwasaidia na kuwalinda watoto walioathirika baada ya kutoka katika maeneo mbalimbali zinatarajiwa kusaidia kutoa elimu zaidi ya kuwandaa kisaikolojia watoto hao ili wasikate tamaa na maisha, pia watoto watalindwa na baadaye watarudishwa kwa wazazi wao kutoka sehemu mbalimbali ndani ya nchi na nje ili waweze kuendelea na majukumu mengine ya kujenga taifa.

Mwisho/-

No comments: