Ukiachana na akina Mange Kimambi, Yericko Nyerere na Malisa GJ waliopewa fedha haramu za madawa kuwasafisha wauzaji madawa mitandaoni kwa kumchafua makonda, binafsi nimeshangazwa sana jinsi Bunge letu tukufu linavyodhoofisha vita ya madawa ya kulevya nchini.
Siamin kama haya ndio maazimio ya bunge zima kwa mtu aliyeweka roho yake rehani ili kuwaokoa vijana wa taifa hili kwa kupambana na madawa ya kulevya nchini….
i) Makonda aitwe bungeni kuhojiwa na Kamati.
ii) Waziri wa TAMISEMI apeleke mwongozo kwa Ma RC na DC kuwa wasiuchezee mhimili wa Bunge.
iii) Mamlaka ya Uteuzi wa RC Dar na DC (yaani Rais Magufuli) zichukue uamuzi haraka kuwavua Madaraka.
iv) Wabunge wanaotuhumiwa wasikamatwe bila kufuata taratibu za bunge.
Mwingine aliyetajwa pia kuhojiwa na Bunge ni DC wa Arumeru - Mh Mnyeti
Mbunge kusimama bungeni na kumchafua mtu bila ushahidi wowote kisa huyo mtu anapambana na maslahi yako(madawa ya kulevya) nje ya bunge ni usaliti kwa taifa, tunajua wabunge wana kinga wa yale wanayoongea bungeni ila tumieni hiyo kinga kuokoa taifa na si kuliharibu taifa. Nilitarajia wangeitumia hiyo kinga kuwataja wafanyabiashara wa madawa ya kulevya, mafisadi, wala rushwa nk ila si kupambana na akina makonda..
Bado siamini kama Bunge letu tukufu limetumia muda wake wa zaid ya masaa 3 kumjadili mpambanaji wa madawa ya kulevya na kumuwekea vikwazo katika mapambano hayo yenye tija kubwa kwa taifa letu
# Bunge linalinda maslahi ya nani katika hili sakata la wafanyabiashara ya madawa ya kulevya????
#tanzaniabilamadawainawezekana
#umojawetundioushindiwetu
2 comments:
If your argument is based on facts, your article lacks legal grounds and/or scientific research to support it. If what you wrote is your personal opinion, then you may be fair in accordance to your limited legal expertise. There is a rule of law in in democratic society. Personally, I support legal actions against illegal drugs. I don't have problems on what Makonda is doing, but I do. on how he is doing. In legal prospective, suspects of wrong doing are arrested or summoned to court based on evidence obtained with regards to the nature of crimes committed. It is prosecutors' job to determine whether the government has enough evidence to charge a suspect and not any political appointee (RC/DC). Leaders who are critical thinkers do not convict citizens on a national television in a broad day light and ask them to meet him or her in such a short notice so that they prove their innocence. Makonda did not need to tarnish images of people who may possibly turn out to be completely innocent. For those who are critical of Makonda are just exercising their constitutional freedom of speech, for we attained independence to do so in 1961. They may have not necessary been paid to do so as your article suggested, bearing in mind that no one have suggested that Makonda Paid you to public-ally trying to silence his critics through your self serving article. If you have evidence to the contrary please feel free to release it. Lastly, the parliament has the right to discipline not only Makonda, but any government leader just like Makonda did to some of their own. That is how democracy works. No one paid me to air my views. I am just exercising freedom of speech.
wewe huna akili kabisa, yaani hatua anazochukua Makonda ndiyo unaona muafaka? Makonda anajitafutia sifa binafsi na wala hana lolote lile, kwa mfano kwa nini asimuweke Masongange kwenye list yake wakati tayari alishawahi kukamatwa live SA akiwa na hayo madawa ya kulevya badala yake anakimbilia kutaja akina Mbowe ili amfurahishe boss wake? Hii kitu bunge naliunga mkono asilimia 100, haiwezekani mtu anakurupuka from no where sababu tu yuko karibu na kiongozi wa nchi na kuanza kuendesha opereshini kubwa kama hiyo, huwezi ukafanya operesheni kubwa kama hiyo peke yako lazima utumie wadau wote wanaohusika, Na hiyo safari ya US Mbona hataki kusema nani alikuw sponsor wake? asitufanye watu wote hatuna akili hapa.
Post a Comment