By Peter Elias, Mwananchi
Dar es Salaam. Rais John Magufuli amemwapisha Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kupambana na Kuzuia Dawa za Kulevya, Rogers Sianga na Kamishna Mkuu wa Uhamiaji, Anna Makakala Ikulu jijiji Dar es Salaam leo.
Rais Magufuli amemtaka Kamishna wa Mamlaka ya kuzuia na kupambana na dawa za kulevya, Rogers Sianga kufanya kazi bila kuogopa ili kuokoa nguvu kazi ya taifa inayoteketea.
Amesema vita ya dawa za kulevya ni ngumu kwa sababu ina faida kubwa na wafanyabiashara hao wanaweza kufanya chochote kwa fedha zao.
"They can do anything at any cost (wanaweza kufanya lolote kwa gharama yoyote). Lazima tushirikiane katika vita hii,' amesema Rais Magufuli.
Pamoja na makamishna hao, Rais pia amewaapisha mabalozi watatu ambao ni Omary Yusuph Mzee (Algeria), Joseph Sokoine (Ubelgiji) na Grace Mgovani (Uganda).

No comments:
Post a Comment