Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kikristo ya Huduma za jamii (CSSC), Peter Maduki.
Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kikristo ya Huduma za jamii (CSSC), Peter Maduki akizungumza na waandishi wa habari. (Picha na Rabi Hume, MO Dewji Blog)
“Makanisa bado yanaendelea kuanzisha na kuendesha taasisi za elimu katika ngazi mbalimbali , hadi mwishoni mwa mwaka 2016, Makanisa yalikuwa yanamiliki taasisi zipatazo 1006. Idadi hii ikiwa ni pamoja na vituo vya Elimu ya Awali vilivyosajiliwa serikalini 300, shule za msingi 172, shule za Sekondari 318, Seminari 52, Vyuo vya Ualimu 11, Vituo vya Mafunzo Stadi 126, Vyuo Vikuu na Vyuo Vikuu Vishiriki 27,” aliongeza mkurugenzi huyo. Akizitaja changamoto wanazokabiliana nazo kwa kipindi chote hicho, mkurugenzi Maduki alisema kuwa Uelewa, Umaskini na Utashi miongoni mwa watendaji na wananchi vimekuwa ni kiwazo kikubwa ambacho hata hivyo alisema wanaendelea kupambana navyo ili kuhakikisha Kanisa linaendelea kutoa huduma zake kwa jamii kwakuwa huo ni wito wake. Tume ya Kikristo ya Huduma za Jamii (CSSC) inaundwa na Baraza la Maaskofu katoliki Tanzania (TEC) na Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) na ilianzishwa mwaka 1992, kwa dhumuni la kuratibu na kusimamia huduma za kijamii zitolewazo na Taasisi za makanisa hususani za Elimu na Afya Nchini.
Kwa miaka mingi sasa, huduma za jamii zitolewazo na makanisa hususani katika sekta ya Afya na Elimu nchini zimekuwa msaada mkubwa kwa wananchi hususani wa maeneo ya vijijini, huku zikiwa na ubora wa kiwango cha juu unaoonekana katika matokeo ya mitihani mbalimbali kwa upande wa elimu na matibabu bora kwa upande wa afya. Alex Mathias,Dar es salaam
No comments:
Post a Comment