ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, February 4, 2017

Mahakama yasitisha amri ya Trump dhidi ya Wahamiaji-BBC

Raia waandamani wakipinga amri ya donald Trump ya kuwazuia Waislamu kutoka mataifa saba kuingia Marekani
Jaji mmoja wa Marekani amesimamisha kwa muda utekelezaji wa amri ya Rais Donald Trump ya kuwazuia raia kutoka mataifa saba, yaliyo na raia wengi wa imani ya Kiislamu kuingia nchini Marekani.

Jaji wa Seattle alipuuzilia mbali sababu zilizotolewa na mawakili wa Serikali na kusema kuwa amri hiyo inaweza kusimamishwa mara moja huku kesi hiyo ikiendelea kusikilizwa mahakamani.

Serikali inatarajiwa kukata rufaa ya dharura dhidi ya uamuzi huo wa mahakama, ambao ni changa moto kubwa kwa utawala wa Trump.

Serikali ya Marekani inasema kuwa makumi ya maelfu ya visa zimefutiliwa mbali tangu rais Trump kutia sahihi amri ya kupunguza idadi ya watu wanaopaswa kuingia nchini Marekani juma lililopita.

Wakati huohuo waziri Mkuu wa zamani wa Norway, Kjell Magne Bondovik, alisema kuwa alizuiwa katika uwanja mmoja wa ndege mapema juma hili, katika tukio alilosema ni la uchokozi, kwa sababu eti alikuwa na visa ya Iran katika paspoti yake.

No comments: