Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Debora Magiligimba amemtaja mtuhumiwa huyo kuwa ni Ntandu Mahumbi (60), mkulima katika kijiji hicho na kwamba tukio hilo ni la Februari 23, mwaka huu saa 5 asubuhi.
“Mtuhumiwa alituambia siku ya tukio yeye alitoka nyumbani kwake kwenda shambani na aliporejea majira ya saa tano asubuhi aliingia ndani na kuchukua panga, akajikata uume wake na kujichoma kwa kisu kifuani ikielezwa ni kutokana na ugumu wa maisha unaomkabili,” amesema Magiligimba.
Amesema polisi inaendelea na uchunguzi ili kufahamu sababu zaidi za mtu huyo kufanya kitendo hicho na mara uchunguzi utakapokamilika, atafikishwa mahakamani.
Hata hivyo, habari ambazo hazikuthibitishwa zinadai kuwa siku ya tukio, Mahumbi aliporudi kutoka shambani alimkuta mke wake akizini na mwanaume mwingine ndani ya nyumba yake, ndipo aliposhikwa na hasira na kuamua kufanya alichotenda.
HABARI LEO
No comments:
Post a Comment